Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

TRC KUCHOCHEA UKUAJI UCHUMI WA NCHI ZA JUMUIYA YA MAENDELEO YA KUSINI MWA AFRIKA - SADC


news title here
15
August
2019

Shirika la Reli Tanzania – TRC limeonekana kuwa chachu ya kukuza uchumi kwa kuendeleza sekta ya miundombinu ya reli nchini katika maadhimisho ya maoneshoya 4 ya wiki ya viwanda ya jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika - SADC ambayo inajumuisha nchi 16 katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere - JNICC jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania – TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amesema kuwa ni fursa kubwa kwa TRC kushiriki katika maadhimisho ya SADC kwa kuonesha na kuelezea huduma zitolewazo na maendeleo ya miradi, ambayo ni mradi mkubwa wa ujenzi ya reli ya kisasa - SGR unaoendelea pamoja na uboreshaji wa reli ya kati Dar – Isaka ambapo itasaidia nchi za jirani kupitisha mizigo kirahisi na haraka zaidi.

“SADC ni soko kubwa na ni sehemu muhimu kwa taifa” amesema Ndugu Masanja Kadogosa.

Ndugu Kadogosa alizungumzia mradi mkubwa unaoendeleawa reli ya kisasa – SGR ambao kwa sasa umefikia asilimia 64.4 na kusema kuwa mradi huo umezingatia vitu mbalimbali ikiwemo mapishano ya barabara ya magari na reli, njia za watembea kwa miguu pamoja na wanyama, vilevile kuweka uzio pembezoni mwa reli ili kuepusha madhara yatakayoweza kutokea.

“Reli hii itajengewa uzio kulia na kushoto kwa asilimia mia moja na shughuli za wananchi za kiuchumi na kijamii zitaendelea kama kawaida” alisema Mkurugenzi Ndugu Masanja Kadogosa.

Ndugu Kadogosa alisema kuwa Usafiri wa Reli ambao ni imara utakabiliana na changamoto ya ushindani wa usafirishaji wa bidhaa za ndani na nje, kuleta chachu ya maendeleo katika uzalishaji na kupunguza gharama za usafiri.

“usafiri wa reli ni nafuu zaidi na unapunguzo asilimia 70 mpaka 60” alisema Ndugu Kadogosa.

Hata hivyo ndugu Kadogosa alisema kuwa TRC ina mpango mzuri wa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari Tanzania kujenga bandari kavu ambayo itasaidia pia nchi jirani ikiwemo Congo kufikisha mizigo ikitokea nchi za nje, na pia shirika la reli limekuwa na juhudi ya kuwa na uhusiano wa karibu na nchi ya Congo kwa kuwa wamekuwa wakishirika vyema katika usafirishaji wa mizigo.

Vilevile Ndugu Kadogosa amewakaribisha mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali kesho Agosti 15 katika maadhimisho hayo ambapo watapata fursa ya kutembelea na kujua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR, mradi ambao unatekelezwa kwa fedha za ndani za watanzania, aidha mabalozi hao watafanya ziara kwenye daraja jipya la Salenda linaloendelea pamoja na kuona mradi wa ufuaji umeme wa Mwalimu Julius Nyerere.