TRC IMESAINI MKATABA WA UNUNUZI WA MASHINE NA MITAMBO YA MATENGENEZO YA NJIA YA SGR
November
2022
Shirika la Reli Tanzania – TRC na Kampuni ya Sung Shin Rolling Stock Technology (SSRST) kutoka nchini Korea Kusini wamesaini mkataba wa ununuzi wa mashine na mitambo ya matengenezo ya njia ya reli ya kisasa – SGR, hafla hiyo imefanyika makao makuu ya TRC jijini Dar es Salaam Novemba 07, 2022.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mhe. Kim Sun Pyo, Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania ambaye ameshuhudia zoezi hilo ameeleza namna nchi ya Korea Kusini ilivyo wekeza kwa muda wa miaka mingi katika uendeshaji wa reli na zaidi ya miaka 30 katika uendeshaji wa reli ya kisasa.
Balozi alibainisha ubora wa Shirika la Reli Korea Kusini pamoja na umahili wa kampuni ya Sung Shin Rolling Stock Technology (SSRST) katika miundombinu ya reli “Shirika la letu la reli likiwa ni namba moja sasa duniani na kampuni hii mnayoingia mkataba ni namba moja kwa utengenezaji wa vyifaa na mitambo ya ukarabati wa njia ya reli duniani”
Barozi aliongeza kuwa usafirishaji wa njia ya reli umekuwa ni uti wa mgongo wa uchumi wa korea kusini kwa zaidi ya karne, na Tanzania ikikamilisha ujenzi wa SGR itaongoza uchumi kwa nchi za Afrika Mashariki na uchumi utakuwa maradufu, mara baada ya kusaini mkataba huu kazi ya utekelezaji itaanza na jambo la muhimu ni ushirikiano na kumaliza kazi kwa wakati.
Naye, Prof. John Kondoro, Mwenyekiti, Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Reli Tanzania alitoa shukrani kwa Selikali ya Jamhuri ya Muungangano wa Tanzania kwa kuendelea kuleta mabadiliko katika Shirika la Reli nchini, kwani reli inayofanya kazi kwa sasa niya muda mrefu hivyo Serikali iliamua kwenda na teknologia ya kisasa kwa kujenga reli ya SGR ambayo itakuwa na kiwango cha kimataifa.
Profesa Kondoro aliongeza kuwa Shirika limekuwa likitumia vibendera na watu kwaajili ya kuangalia na kukagua usalama wa njia ya reli na sasa kupitia mkataba huu katika reli ya SGR inaenda kutumia teknologia ya kisasa katika mashine ya ukaguzi wa njia, mtambo wa kukagua mipasuko ya ndani ya reli pamoja na mashine ya kupigilia.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu TRC Masanja kadogosa alisema kuwa lengo la ununuzi wa mashine na mitambo hii, ni kuongeza ufanisi wa matengenezo ya njia na kupunguza kufanya matengenezo ya njia kwa kutumia watu. Ambapo mitambo hiyo itaipa uwezo TRC katika kutunza njia ya SGR muda wote wa uendeshaji.
Katika hatua nyingine Mkrugenzi Mkuu TRC ameainisha kuwa mkataba huu utahususha ununuzi wa mashine na mitambo ambayo ni mtambo wa kuunganisha Reli, mashine ya ukaguzi wa njia, mtambo wa kukagua mipasuko ya ndani ya reli, mashine ya kupigilia mashine za kupigilia, viberenge vya uwezo mkubwa vya kubeba mizigo wakati wa matengenezo, gari linalotumika wakati wa ukaguzi wa njia, gari la ukaguzi wa madaraja, mtambo wa kuua majani yanayoota pembeni ya Reli, mtambo wa kuzima moto sehemu mbalimbali za Reli ikiwemo mahandaki, gari la kukagua miundombinu ya umeme, gari la matengenezo ya miundombinu ya umeme, na mashine ya kukaza vifungio.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu TRC amesema kununua mashine na mitambo tofauti ishirini na nne (24), itagharimu jumla ya Dola za Marekani Millioni 51, utekelezaji wa mkataba utahusisha utengenezaji, mafunzo, na makabidhiano unatarajiwa kufanyika kwa miezi kumi na mbili (12). Sambamba na ununuzi huo, tayari Shirika limeandaa wafanyakazi watakaofundishwa namna bora ya kutumia mashine na mitambo hiyo kwa ufanisi.