Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

SHIRIKA LA RELI TANZANIA - TRC LIMEKABIDHI BEHEWA 40 KWA SHIRIKA LA MPANGO WA CHAKULA DUNIANI - WFP


news title here
18
February
2021

Shirika la reli Tanzania – TRC limekabidhi behewa 40 za mizigo kwa Shirika la mpango wa chakula duniani - WFP katika hafla fupi iliyofanyika katika kituo cha mizigo Ilala jijini Dar es Salaam Februari 17, 2021.

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Naibu Waziri Wa Ujenzi NaUchukuzi Mh. Godfrey Kasekenya ,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC Profesa John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu TRC Ndugu Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mkazi - WFP Bi. Sarah Gordon, Uongozi wa Shirika la Reli Tanzania, Wafanyakazi TRC Wawakilishi kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani - WFP Wadau wa TRC na WFP, Pamoja na Wanahabari.

Lengo la kukarabati mabehewa 40 ni Kudumisha uhusiano wa kibiashara uliodumu kwa muda mrefu kati ya TRC na WFP na Kuongeza uwezo wa usafirishaji wa Mizigo ya WFP kwa njia ya reli na kuifanya sekta ya reli kuwa kichochea katika ukuaji wauchumi wa Nchi na kupelekea Tanzania kuendelea kufanya vizuri kiuchumi.

Aidha Shirika la Reli Nchini limekuwa na ushirikiano na baadhi ya wadau mbalimbali wakiwemo Shirika la chakula Duniani (WFP), wadau hao wameshiriki kikamilifu kwa kufanya ukarabati wa mabehewaambayo hutumika katika kusafirisha mizigo yao lakini pia hutumika kuhudumia mizigo ya wasafirishaji wengine jambo ambalo limesaidia kuongeza ufanisi wenye tija kwa kwa Shirika la Reli katika kuhudumia mizigo hususani inayotoka katika Bandari ya Dar es Salaam.

Mgeni Rasmi Naibu Waziri Wa Ujenzi NaUchukuzi Mh. Godfrey Kasekenya, ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Shirika la reli pamoja na wadau katika kuimalisha sekta ya reli kwa kukarabati behewa ili kuongeza ufanisi katika kuhuma za usafirishaji wa mizigo.

“Naishukuru Serikali ya awamu ya tano ilipo ingia madarakani ilijikita kuinua Shirika la reli nchini ambapo ilitoa kiasi cha Shilingi Bilioni 4 (nne) za kitanzania kwa ajili ya kukarabati behewa 200, ambapo kwa sasa nimetaarifiwa jumla ya mabehewa 162 yameshakarabatiwa na behewa 38 zinaendelea kwa ukarabati” alisema Naibu Waziri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi - TRC Prof. John Kondoro, alibainisha uhusiano uliopo kati ya TRC na WFP kuwa ni maagizo ya Wizara yenye dhamana katika kuhakikisha Serikali kwa kushirikiana na Shirika inashirikisha wadau mbalimbali na wafanyabishara.

“Ushirika huu ni utekelezaji wa melekezo ya Wizara tuweze kushirikisha wadau na wafanyabiasha ili tuweze kuimarisha shirika letu. Tunaendelea kushirikisha wadau wengine na huu ni mwanzo kamba leo tunashuhudia makabidhiano ya behewa 40 ambazo zimegharamiwana WFP tutaendelea kushirikisha wadau wengine kwa kuwa uhitaji wa mabehewa ni mkubwa sana” alisema Prof. Kondoro.

Naye Mkurugenzi Mkuu TRC, alitoa takwimu ya behewa zilizokamilika kukarabatiwa na zinazohitajika kukarabatiwa sambamba na kutoa wito kwa wadau wengine wa usafirishaji kuendelea kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais John Pombe Magufuli za kuimarisha sekta ya reli nchini.

“Behewa zinazohitajika kufanyiwa ukarabati mkubwa ni 500, ambapo behewa 200 tayari zinagharamiwa na Serikali. Takribani behewa 300 zinahitaji kukarabatiwa, kutokana na hilo bado TRC inajukumu la kuboresha behewa hizo na tunaendelea kukaribisha wadau katika sekta mbalimbali tushirikiane kwa pamoja kuunga mkono juhudi za Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kukarabati behewa zilizobaki” alisema Mkurugenzi Mkuu.

Hata hivyo Mkurugenzi Mkazi - WFP Bi. Sarah Gordon alieleza namna WFP ilivyo shiriki kuinua uchumi wa usafirishaji nchini kupitia sekta ya reli ndani ya miaka miwili, ambapo alieleza pia maono ya ushirikiano huo utakavyoleta tija kiuchumi katika siku za mbeleni.

“Mwaka 2018 mpaka 2020 WFP ilinunua hapa nchini bidhaa za chakula tani za uzito 262,000 na kuiingizia uchumi wa nchi jumla ya dola za kimarekani milioni 160 kutokana na manunuzi pamoja na huduma ya usafirishaji wa tani hizo, nimatumaini yetu kwamba uhusiano huu wa kiabiasha utaendelea kukua hata kwa siku zijazo” alisema Bi. Sarah Gordon.

Ushirikiano uliopo kati ya wadau wa sekta ya reli nchini, wafanyabiashara pamoja na Shirika la reli Tanzania ni kiungo kikubwa katika kuleta maendeleo ya uchumi wa usafirishaji nchini ambapo WFP wameonesha nia na faida imeonekana kwa sasa na hata kwa siku zijazo katika kuongeza ufanisi wa utendaji kazi ndani nan je ya nchi.