Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

SHIRIKA LA RELI TANZANIA – TRC LASHIRIKI MAONESHO YA NNE YA (SADC)


news title here
08
August
2019

SHIRIKA LA RELI TANZANIA – TRC LASHIRIKI MAONESHO YA NNE YA WIKI YA VIWANDA YA JAMUIA YA MAENDELEO YA KUSINI MWA AFRIKA (SADC)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa atembelea Banda la Shirika la Reli Tanzania –TRC katika maazimisho ya maonesho ya nne ya wiki ya viwanda ya jamuia ya maendeleo ya kusini mwa afrika (SADC) ambazo ni nchi 16 yaliyofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam,6 Agosti,2019.

Aidha, waziri mkuu ametoa pongezi za dhati kwa shirika la Reli nchini kwa usimamizi mzuri wa mradi mkubwa wa kitaifa wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR unaoendelea kujengwa nchini. “TRC inaonekana kama mmejipanga vizuri“ waziri Majariwa alisema.

Katika maonesho hayo jumla ya nchi 16 za jamuia ya maendeleo ya kusini mwa afrika (SADC) zimehudhuria ambazo ni Tanzania, DRC Congo, Angola, Lesotho, Malawi. Madagascar, Mauritus, Mozambique, Namibia, South Africa, Seychelle, Swaziland, Zimbabwe, Zambia, Comoros,

Halikadhalika, maonesho ya SADC yamewawezesha wananchi wa Tanzania na wageni wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC) ambazo ni nchi kumi na sita, kupata fursa mbalimbali ikiwemo kujua miradi mikubwa ya kitaifa ya kimkakati inayosimamiwa na Shirika la Reli Nchini ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa SGR awamu ya kwanza Dar es Salaam – Morogoro ambapo ujenzi umefikia asilimia 60,

Awamu ya pili ya ujenzi Morogoro – Matukupola ambapo ujenzi umefikia zaidi ya asilimia 14 pia Shirika linasimamia mradi wa uboreshaji wa reli ya kati Dar es Salaam Mpaka Isaka Km 970 –TIRP ambao ujenzi wake umefikia zaidi ya asilimia 34 na ufunguzi wa njia ya Reli ya Tanga, Moshi na Arusha ambapo safari za mizigo zilizinduliwa rasmi mwishoni wa mwezi wa saba.

Hivyohivyo, Maonesho haya ya viwanda ni fursa kwa Shirika la Reli Nchini kwani kupitia sekta ya uchukuzi na usafirishaji kwa njia ya reli itaongeza wigo wa masoko ya ndani na nje ya nchi. Reli hii ya kisasa itayojengwa itakuwa na faida kubwa kiuchumi nje na ndani ya nchi kwani itachochea maendeleo katika sekta ya kilimo, viwanda, biashara na madini hususani maeneo ambayo reli itapita pamoja na kwa nchi jirani hasa DRC.