SHIRIKA LA RELI TANZANIA – TRC LAREJESHA HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI ZA MIZIGO

February
2020
SHIRIKA LA RELI TANZANIA – TRC LAREJESHA HUDUMA YA USAFIRI WA TRENI ZA MIZIGO
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ngudu Masanja Kungu Kadogosa amefanya mahojiano ya ana kwa ana na wanahabari kutoka kituo cha habari cha AZAM TV kuhusu kurejesha huduma ya usafiri reli ya kati baada ya Shirika kusitisha kutoa huduma takribani siku 20 kutokana na miundombinu ya reli kuharibika katika eneo la kilosa Gulwe Mkoani Morogoro, uharibifu huo ulisababishwa na mvua kubwa zilizotajwa kunyesha kwa wingi katika Mikoa ya Iringa, Manyara ,Singida na Dodoma na hivyo kupelekea maji kuwa mengi na kuharibu miundombinu ya reli. Mahojiano yamefanyika katika ofisi ya Mkurungenzi Mkuu makao makuu jijini Dar es Salaam, januari 26, 2020.
Aidha, Mapema mwezi januari 2020 Shirika lilistisha kutoa huduma za usafiri wa abiria na mizigo kwa reli ya kati kutokana na mvua zilizoendelea kunyesha na kupelekea kuharibu miundimbinu ya reli umbali wa kilomita 120, ikiwemo kuharibika kwa makaravati, reli, station, na madaraja. Hata hivyo Jitihada zilifanyika kwa kasi kutoka kwa wahandisi wa TRC, na wahandisi wa wamkandarasi kampuni za CCECC pamoja na mkandarasi YAPI MARKEZI ambao wameshirikiana na hatimaye kukamilisha na kurejesha huduma ya usafirishaji kwa njia ya reli, na huduma imerejeshwa februari 22, 2020.
Mkurugenzi Mkuu, amebainisha namna Shirika lilivyoanza kutoa huduma kwa kupitisha treni za mizigo ambayo matenki ya mafuta ikifatiwa na treni ya mizigo mbalimbali ambazo kupitishwa kwa lengo la kupima ubora wa njia kabla ya treni ya abiria kupita. Aidha Shirika limeanza kutoa huduma kwa kupitisha treni za mizigo ambazo zimebeba matanki 56 ya mafuta na tani 16 za seruji na nondo.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu amesema kuwa njia iliyofunguliwa ni ya muda kutokana na uhitaji wa wateja wa mizigo kuwa mkubwa, hata hivyo jumla ya bilioni 1 imetumika katika kujenga njia ya muda na kuruhusu huduma kuendelea. Aidha Shirika kwa sasa limejikita kujenga njia ya kudumu ambayo itakuwa ni suruhisho la athari ya mvua zinazotokea na kuharibu miundombinu ya reli katika maeneo ya kilosa, ambapo bilioni 6 zimetengwa kwa ajili ya kujenga njia ya kudumu.
Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mkuu ameweka wazi namna Shirika lilivyo ingia hasara baada ya kusitisha huduma kwa takribani siku 20 ambapo shirika huingiza pato la shilingi milioni 150 kwa siku hivyo kupelekea kupoteza fedha nyingi zaidi ya bilioni 3. Hata hivyo Shirika limejipanga vyema katika kutoa huduma ikiwemo kujenga njia ya muda ili kuruhusu mizigo kufika kwa wateja pamoja na kuongeza idadi ya treni za mizigo ili kuhakikisha idadi kubwa ya mizingo inasafirishwa kwa wakati.