Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SHIRIKA LA RELI TANZANIA – TRC LAENDELEA NA ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA MKOANI MOROGORO


news title here
25
February
2020

SHIRIKA LA RELI TANZANIA – TRC LAENDELEA NA ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA MKOANI MOROGORO

Shirika la Reli Tanzania – TRC laendelea na zoezi la ulipaji wa fidia kwa wananchi waliotwaliwa rasilimali zao kwa lengo la kupisha ujenzi wa reli ya kisasa – SGR kwa awamu ya Pili Morogoro – Makutupora, hivi karibuni Februari 2020.

Zoezi linaendelea katika mikoa yote iliyopitiwa na mradi wa ujenzi wa reli kisasa Morogoro – Makutupora wenye mtandao wa KM 422 ambapo ujenzi unaendelea kwa kasi ukifikia zaidi ya asilimia 25.

Aidha, zoezi la ulipaji fidia linaendelea katika Wilaya ya Kilosa na Mvomelo Mkoani Morogoro katika Vijiji vya Kimambila, Chanzuru, Mkwatani, Kasiki, Mwasa, Kondoa na Mkadage ambapo wananchi wamelipwa fidia zao ili kupisha ujenzi wa reli ya kisasa – SGR punde tu wanapopokea hundi ya malipo na kuwataka ndani ya siku 14 kupisha eneo na mkandarasi kuendelea na ujenzi.

Malipo ya fidia yanapofanyika, viongozi wa ngazi ya kijiji, kata mpaka mkoa hutoa elimu ya matuumizi bora ya fedha hizo hasa katika kuleta maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

Fidia zinazolipwa ni fidia ya ardhi, nyumba, miti, mazao na maeneo yaliyotwaliwa kwa ajili ya kuchimba vifusi na kumwaga ambapo Serikali kupitia Shirika la Reli hutoa fedha kwa walengwa kama fidia.

Zoezi hili huendeshwa na maafisa kutoka Shirika la Reli Tanzania wakishirikiana na viongozi wakata, vijiji, Hamashauri na Wilaya na kusimamiwa na vyombo vya usalama kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

Kwa upande mwingine, viongozi wa vijiji na kata wamelishukuru Shirika kwa Kutimiza ahadi ya kuwalipa wananchi stahiki zao, hata hivyo viongozi hao walitoa neno juu ya zoezi la fidia kwa kuwapongeza maafisa wa Shirika la Reli kwa kuendesha zoezi kwa muda sahihi na kwa ufanisi huku amani na usalama ukiwepo eneo la tukio, pia wamewaomba wananchi kutumia fedha kwa maendeleo ya familia zao

Nao wananchi hawakuwa nyuma kutoa pongezi na shukurani kwa Serikali kupitia Shirika kwa kutimiza ahadi ya kulipa fidia kwa wakati na kuonesha kufurahia mradi huo kwani umekuwa ni fursa kwa wakazi wa maeneo hayo ambapo vijana wamejipatia ajira mbalimbali huku wengine wakijikita katika fulsa ya biashara ndogondogo