Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

SHIRIKA LA RELI TANZANIA - TRC LAENDELEA NA ZOEZI LA KUHAMISHA MAKABURI.


news title here
16
November
2020

Shirika la Reli Tanzania - TRC laendelea na zoezi la kuhamisha makaburi katika Wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro katika kijiji cha Munisagara ili kupisha Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR.Kazi ya kuhamisha Makaburi haya Umefanyika rasmi hivi karibuni Novemba 2020.Kazi hiyo ya kuhamisha makaburi inafanywa na wafanyakazi wa TRC kwa kushirikiana na maafisa kutoka wilaya ya Kilosa na wanakijiji husika ili kuepusha malalamiko kwa wakazi wa maeneo hayo.Msimamizi wa Maswala ya Kijamii kutoka TRC Ndugu. Joyce Ponera akiongea na wananchi wa kijiji cha Munisagara “amesema kuwa Wananchi msiwe na wasiwasi na uhamishaji wa makaburi ni jambo la kawaida na hivyo wasione kama wameonewa na Serikali, Serikali inamipango mizuri ya kuendeleza miundombinu hivyo wajitoe kuunga maamuzi ya Mh.Rais Dr.John Pombe Magufuli katika uboreshaji miundombinu Nchini kwa maslahi ya Taifa”.Aidha wananchi wanaombwa na TRC kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo na kumpisha mkandarasi kuendelea na ujenzi ili kumaliza ujenzi kwa muda uliopangwa katika makubaliano ya Mkataba.Pia wameobwa kuwa na Subira na Shirika la Reli Tanzania - TRC wameahidi kulipa fidia ya makaburi hayo mapema iwezekanavyo ili kutoleta usumbufu kwa ndugu na jamaa wa makaburi hayo.