Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

SHIRIKA LA RELI TANZANIA - TRC LAENDELEA NA ZOEZI LA KUHAMISHA MAKABURI KIPANDE CHA MOROGORO - MAKUTUPORA


news title here
24
August
2019

Shirika la Reli Tanzania - TRC laendelea na zoezi la kuhamisha makaburi katika Wilaya ya Mpwapwa Mkoa wa Dodoma katika Vijiji vya Gulwe, Godegode,Msagali na Kikundi ili kupisha Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR.Kazi ya kuhamisha Makaburi imeanza rasmi hivi karibuni Agosti 2019.

Kazi hii ya kuhamisha Makaburi inafanyika katika kipande cha Pili cha ujenzi wa Reli ya kisasa Morogoro - Makutupora ambao sasa ujenzi umefikia zaidi ya asilimia 13.

Ni katribani makaburi 200 yataondolewa na kwenda kuzikwa kwenye maeneo rasmi yaliyopangwa na Serikali .

Kazi hiyo ya kuhamisha makaburi inafanywa na wafanyakazi wa TRC kwa kushirikiana na maafisa kutoka wilaya ya Mpwapwa na za vijiji husika ili kuepusha malalamiko kwa wakazi wa maeneo hayo.

Akiongea na wananchi Afisa Afya wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Aizak Lwiza “amesema kuwa Wananchi msiwe na wasiwasi na uhamishaji wa makaburi ni jambo la kawaida na hivyo wasione kama wameonewa na Serikali, Serikali inamipango mizuri ya kuendeleza miundombinu hivyo wajitoe kuunga maamuzi ya Mh.Rais Dr.John Pombe Magufuli katika unoreshajinwa miundombinu Nchini kwa maslahi ya Taifa.

Aidha wananchi wanaombwa na TRC kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo na kumpisha mkandarasi kuendelea na ujenzi ili kumaliza ujenzi kwa mda uliopangwa katika makubaliano ya Mkataba.

Pia wameobwa kuwa na Subira na Shirika la Reli Tanzania - TRC wameahidi kulipa fidia ya makaburi hayo mapema iwezekanavyo ili kutoleta usumbufu kwa ndugu na jamaa wa makaburi hayo.