Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SHIRIKA LA RELI TANZANIA NA CHUO CHA TAIFA CHA USAFIRISHAJI WASHIRIKIANA KITAALUMA


news title here
14
August
2020


Shirika la Reli Tanzania – TRC na Baraza la Uongozi Chuo cha Taifa cha Usafirishaji – NIT wamefanya mazungumzo huku lengo likiwa kuimalisha uhusiano baina yao sambamba na kuona changamoto ya rasilimali watu katika taaluma ya reli. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Reli Tanzania, Jijini Dar es Salaam Agosti 13, 2020.

Mazungumzo hayo yameendeshwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Ndugu Masanja Kungu Kadogosa na Mkuu wa Cha Usafirishaji Mhandisi prof. Zacharia Mganilwa pamoja na Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mazungumzo hayo yalijikita katika makubaliano ya kuendeleza uhusiano na ushirikiano baina yao wakiwa kama wadau wakubwa wa sekta ya usafirishaji nchini lakini pia kuanzisha na kuendeleza mitaala ya taaluma ya sekta ya reli ili kuongeza wataalamu nchini hasa katika kipindi ambacho Taifa limeingia katika uchumi wa kati.

Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini amezungumzia mchango unaoendelea kutolewa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji katika kutoa wataalamu mbalimbali nchini katika sekta ya usafirishaji pamoja na ushiriki wa Shirika la Reli kitaaluma katika kuandaa mitaala ya kufundishia wanafuzi, ambapo kimsingi imekuwa ni chachu ya kukuza sekta ya reli lakini pia katika kujenga uhusiano wa karibu na wenye tija katika maendeleo ya Taifa kupitia usafirishaji na uchukuzi.

“Sisi kama Shirika kazi yetu ni kusafirisha na wao kama Chuo ni kutoa wataalamu ambao watakuja kusimamia uendeshaji wa reli, kwa hiyo hiki ni chuo ambacho ni mhimu sana kwa Shirika, na tumeshirikiana nao katika kuandaa mitaala ya kufundishia taaluma ya reli. Kuwa na reli ambayo ni endelevu tunahitaji kuwa na watalamu pamoja na chuo kutokana na ujenzi wa reli kuwa endelevu” Ndugu Kadogosa aliema.

Kwa upande wake, Prof, Mhandisi Mganilwa alibainisha changamo iliyopo katika Sekta ya reli kwa upande wa rasilimali watu katika wataalam ya mambo ya reli, hivyo kuona kuwa kuna umuhimu wa kuanzisha mitaala ya usimamizi wa usafirishaji kwa njia ya reli katika chuo cha Usafirishaji chaTaifa kwa lengo la kuzalisha wataalamu wengi nchini ambao wataisaidia serikali kuendeleza sekta ya reli hasa katika reli ya kisasa – SGR.

“kwa sasa Tanzania hatuna wataalaamu wa kutosha katika taaaluma ya mambo ya reli, sasa tunaelekea kuanza kuzalisha wataalaamu hapa hapa nchini ili wakizalishwa kwa wengi waweze kusimamia miundombinu ya usafirishaji. Matarajio yetu baada ya kuanza kufundisha hao wataalamu kwa maana ya mafundi na wahandisi watapata fulsa ya kuja kufanya mazoezi kwa vitendo na baadae kuajiliwa na shirika kwa manufaa ya Taifa letu’’ Mkuu wa Chuo alisema.

Katika hatua nyingine, Baraza la Uongozi Chuo cha Taifa cha Usafirishaji – NIT walipata fursa ya kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR kutoka Dar es Salaam mpaka Kilosa umbali wa KM 278 wakiongozwa na Meneja Mradi Msaidizi Ayoub Mdachi. Wakati wa ziara Baraza la Uongozi wa Chuo lilipata kujionea hatua mblimbali za ujenzi ikiwemo ujenzi wa tuta, madaraja, vivuko, uchomeleaji wa reli, pamoja na ukaguzi wa mahandaki yanayoelekea kukamilika ujenzi wake.

Wajumbe hao walifurahishwa na kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano huku wakilipongeza Shirika kwa kusimamia mradi mkubwa kwa kushirikiana na makampuni ya ndani ya nchi na nje.

Vile vile, Mkuu wa Chuo alipata fursa ya kuelezea namna reli hii ya kisasa na reli ya kati zilivyo na mchango mkubwa hasa wakati ambapo Taifa la Tanzania limeingia katika uchumi wa kati.

“Tunapozungumzia Tanzania kuingia katika uchumi wa kati maana yake ni Taifa lililoendelea, umefanikiwa kuunganisha mikoa yote ya Tanzania bara kwa barabara za lami kinachofuta sasa ni kuunganisha mikoa yote, katika miaka 10 ijayo tuna majiji 6 matarajio ni kwamba majiji hayo yatakuwa na usafiri wa reli ya umeme na hapo tutaweza kusafirisha abiria na mizigo na uchumi wa viwanda utafanya malighafi zisafirishwe kwenye viwanda na bidhaa zinazotengenezwa ziwafikie walaji na bidhaa zinazotengenezwa viwandani zifike sokoni kwa haraka ndani na nje ya nchi” Prof Mganila alisema.