Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SHIRIKA LA RELI TANZANIA LASITISHA HAFLA YA KUKABIDHI BEHEWA 40 ZA MIZIGO KUTOKANA NA UGONJWA WA CORONA


news title here
17
March
2020

Shirika la Reli Tanzania – TRC lasitisha hafla ya kukabidhi Behewa 40 za Mizigo kufuatia agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim la kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona lililotolewa leo Machi 17, 2020.

Hafla hiyo iliyopangwa kufanyika Machi 18, 2020 kwa lengo la kukabidhi Behewa 40 za Mizigo kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP zilizokarabatiwa kwa ushirikiano kati ya TRC na WFP ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma ya usafirishaji wa Mizigo kati ya Bandari ya Dar es Salaam, Uganda, Congo na Burundi.

Akizungumza kwa niaba ya Uongozi wa Shirika Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano Bi Jamila Mbarouk ameeleza kuwa uongozi wa Shirika la Reli Tanzania unaunga mkono jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kupambana dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona kwa maslahi ya watanzania ambapo leo Shirika limesitisha hafla ya kukabidhi behewa 40 kwa WFP, pia ametoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

“Kwa sasa tumesitisha zoezi hili mpaka hali itakapokaa sawa, tuko tayari kuilinda nguvukazi ya Tanzania na kuchukua tahadhari” alisema Jamila.

Jamila aliendelea kusisitiza wananchi watanzania kuunga mkono juhudi za serikali kuzuia maambukizi kuacha kushiriki katika mikusanyiko ya watu wengi kama mikutano ya kisasa, semina, Hafla mbalimbali na sherehe za harusi kwa maslahi ya Taifa.