Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SHIRIKA LA RELI TANZANIA LASHIRIKI MAONESHO YA 23 YA USAFIRISHAJI BARANI AFRIKA


news title here
16
January
2020


Shirika la Reli Tanzania – TRC lashiriki Mkutano na Maonesho ya 23 ya usafirishaji barani Afrika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam Januari 15 - 16, 2020.

Maonesho na Mkutano hayo yamefanyika kwa lengo la kuwakutanisha wadau wa sekta ya usafirishaji kuonesha huduma na bidhaa zao pamoja na kujadili namna ya kuboresha sekta usafirishaji barani Afrika.

Aidha, maonesho hayo yamefunguliwa rasmi na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe na kusema kuwa Serikali ya awamu ya tano inatekeleza Miradi mikubwa katika sekta ya uchukuzi ikiwemo miradi miwili ya reli ambayo ni ujenzi wa reli ya kisasa – SGR na uboreshaji wa reli ya kati - TIRP ambayo kwa pamoja itasaidia kusafirisha mizigo kwa wingi na haraka zaidi ndani ya Tanzania na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Congo.

Kampuni zipatazo 18 zinazojihusisha na usafiri wa ardhini na majini zinashiriki maonesho hayo yanayofanyika kila mwaka ambapo mwaka huu yamefanyika nchini Tanzania

Miongoni mwa Mashirika yaliyoshiriki ni pamoja na Mamlaka ya Bandari Tanzania – TPA, Shirika la Wakala wa Usafiri Majini – TASAC, Mamlaka ya Usafiri Ardhini – LATRA, Mamlaka ya Bandari Kenya, Shirika la Reli Tanzania pamoja na kampuni nyingine kutoka nje zinazojishughulisha na usafirishaji barani Afrika.

Hata hivyo Waziri Kamwelwe amewashukuru waandaaji wa maonesho hayo kwa kuamua kufanya mkutano huo nchini Tanzania, na kuongeza kuwa Tanzania inawakaribisha wawekezaji na wadau wengine wa sekta ya usafirishaji kuwekeza katika sekta ya uchukuzi