Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

SHIRIKA LA RELI TANZANIA LAFANYA KAMPENI YA UELEWA NDANI YA TRENI YA DELUXE KUTOKA DAR ES SALAAM MPAKA MOSHI


news title here
03
February
2020

Shirika la Reli Tanzania - TRC linaendelea na kampeni ya uelewa kuzuia ajali na hujuma dhidi ya miundombinu ya reli kwa kutoa elimu kuhusu mambo ya kuzingatia katika maeneo ya miundombinu ya reli kwa abiria wa treni ya Deluxe Dar es Salaam – Moshi, hivi karibuni Februari 2020.

Hivi karibuni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Focus Sahani alizindua Kampeni hiyo yenye lengo la kutoa elimu ya uelewa juu ya mambo kadhaa yanayohusu kuzuia ajali na hujuma dhidi ya miundombinu ya reli ikiwemo matumizi sahihi ya alama za reli, mfumo wa kushughulikia maoni, malalamiko na taarifa zinazoripotiwa kuhusu hujuma dhidi ya miundombinu ya reli.

Kampeni hii ni endelevu ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka ili kuhimiza utunzaji wa miundombinu ya reli ambapo mwaka huu Shirika limejikita katika kuboresha namna ya ufikishaji elimu na taarifu kuhusu masuala hayo kupitia njia tofauti ikiwemo Mikutano ya ana kwa ana na wananchi, kupitia vyombo vya habari sambamba na mbinu mpya ya kuwafuata abiria katika treni na kuwapatia elimu hiyo.

Zoezi hilo la kutoa elimu ya uelewa liliambatana na utoaji zawadi kwa abiria ambao wamekuwa wakijibu maswali ambayo waliulizwa na Maafisa kutoka TRC kuhusu Usalama wa reli, Shirika linaamini kwamba wananchi ndio walinzi wakuu wa miundombinu ya reli kwa kuanza na mmoja mmoja hadi jamii nzima hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwafikishia elimu na taarifa kuhusu namna ya kutunza miundombinu ya reli.

Kwa upande mwingine abiria walilipongeza Shirika kwa kuendelea kutoa elimu ya ya uelewa kuhusu ulinzi na kutunza miundombinu ya reli, pia abiria walipata fursa ya kutoa maoni na ushauri kwa Shirika namna jamii inavyoweza kushirikiana na Serikali za mitaa kuzuia ajali na hujuma dhidi ya miundombinu ya reli.

“Binafsi naipongeza Serikali kupitia Shirika la reli kwa kuendelea kuimarisha miundombinu ya reli kwa kurejesha safari za Mikoa ya kaskasini ambapo kwa muda mrefu hatukuwa na usafiri huu ambao ni mzuri, salama na wa gharama nafuu, nitoe wito kwa wananchi tutunze reli yetu ili iendelee kutusaidia na6 kutuimarishia uchumi hasa kwa sisi wafanyabiashara pia ningeomba serikali za mitaa ziweke ulinzi shirikishi kubaini wanaohujumu reli” alisema abiria Nasra Moses