Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SHIRIKA LA RELI TANZANIA LAENDELEA NA KAMPENI YA UELEWA KUHUSU MIRADI INAYOSIMAMIWA NA TRC.


news title here
16
December
2019

Wakati Shirika la Reli Tanzania -TRC linaendelea kuadhimisha Wiki ya TRC kwa kutembelea vyombo vya habari tofauti Nchini, Timu ya mawasiliano kutoka TRC inaendelea na kampeni ya kuwapatia wananchi uelewa kuhusu miradi inayosimamiwa na TRC ikiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR ,ukarabati wa Reli ya kati inayoanzia Dar Es Salaam hadi Isaka km 970 na Mradi wa ufufuaji wa reli ya Tanga Moshi na Arusha ambao hadi sasa umezaa matunda kutokana na kurejea kwa huduma ya usafiri ambao ulikuwa umesimama kwa takribani miaka 25, kampeni hiyo iilianza rasmi tarehe 1 desemba 2019.

Lengo la kampeni hii ni kukutana na wananchi kuwapa uelewa na kuwakumbusha umuhimu wa kulinda miundombinu ya Reli na kwa kiasi gani wananchi wameshirikishwa kwenye miradi inavyoendelea TRC.

Uwepo wa miradi hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kwa wananchi watanzania kuweza kupata fursa za ajira kwa mradi wa uboreshaji wa reli ya kati watanzania 1600 wamepata ajira na upande wa SGR zaidi ya watanzania 14000, hali hii inaonesha dhahiri faida za miradi hii.

Kwa mkoa wa pwani Dar Es salaam timu ya mawasiliano kutoka TRC ilifika Katika maeneo mbalimbali Vingunguti,kipawa Pugu na Mpiji na kisha kuendelea katika vijiji vya Mkoa wa pwani ikiwemo Mpiji na morogoro.

Timu hiyo iliendelea na kampeni hiyo kufika kijiji cha Mikese Mkoani Morogoro ambapo wananchi waliweza kuzungumzia changamoto ya ukosefu wa vivuko katika maeneo ya reli jambo ambalo linawapa changamoto.

Maeneo mengine ambayo timu hii imeyatembelea ni pamoja na Kilosa katika Vijiji vya Mkadage,Kilosa Uwanja wa Behewa kijiji cha mwasa na maeneo mengine ya kuelekea Dodoma.

Katika kampeni wananchi waliweza kupata nafasi ya kuuliza maswali na kuelezea changamoto huku wengine wakiongeza utendaji wa shirika kwa utendaji wa kampeni hii na kutembelea maeneo ambayo reli inapiga kukutana na wananchi.

Katika kampeni wataalam wa masuala ya kijamii walitoa Elimu za afya na kujilinda na mgonjwa ya maambukizi lakini pia wananchi alipata fursa ya kupima afya zao kupata majibu hapohapo.

Wataalamu wameeleza kuwa uwepo wa miradi hii huchangia ongezeko la watu wengi hivyo hakuna budi wananchi kujilinda na maambukizi ya ukimwi.

Pia kampeni hii imeweza kukutana na wafanyakazi wanaoboresha reli ya kutoka Daresalaam hadi isaka maeneo ya kintinku Manyoni ambao nao kwa namna moja ama nyingine wameweza kugusia baadhi ya changamoto .

Kampeni hii ilianza rasmi mwanzoni mwa mwezi wa 12, yenye lengo la kutembelea maeneo ambayo reli inapiga ili kutoa Elimu mbalimbali zinazohusu miradi,huduma zitolewazo na TRC, afya na kuomba ushirikiano wa karibu kwa wananchi katika ulinzi wa miundo mbinu ya reli, na jukum la ulinzi ni letu sote.Kwa yeyote atakaekamatwa na miundo mbinu ya reli hatua kali za kisheria zitatekelezwa.