Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

SHIRIKA LA RELI TANZANIA KUTOA FURSA KWA WATEJA WA AIRTEL KUNUNUA TIKETI MTANDAONI


news title here
14
December
2020

Shirika la Ŕeli Tanzania - TRC limetoa fursa kwa wateja wa kampuni ya mtandao wa simu AIRTEL kwa kuwarahisishia huduma za ukataji tiketi kwa njia ya mtandao katika kipindi cha msimu wa sikukuu za Christmas na Mwaka mpya kwa wateja, wakati wa mkutano wa wandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano makao makuu TRC, hivi karibuni Disemba 2020.

Aidha, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania imetoa fursa kwa wateja wake kulipia tiketi za TRC kupitia kiunganishi cha malipo ya serikali ambapo wataweza kununua tiketi za kusafiri kwa treni kupitia akaunti zao za Airtel Money, hivyo itawasaidia wateja kupunguza changamoto za kwenda stesheni na kupanga foleni ili kukata tiketi.

Mkurugenzi Mkuu TRC amebainisha kuwa Kwa kuwapatia wateja fursa hiyo na Airtel Tanzania itasaidia kuboresha zaidi utoaji huduma kwa wateja wanaotumia mtandao wakati wakulipia tiketi zao kwani ni rahisi kwenye kutumia na vile vile unaweza kujihudumia ukiwa popote na hivyo kuwahakikishia wateja huduma za uhakika na haraka.

“Naendelea kuwasihi wateja wetu tukate tiketi kwa njia ya mtandao ambayo ni rahisi zaidi popote ulipo, maana ni inakupunguzia garama na muda” alisema Ndugu Kadogosa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Airtel Money Beatrice Singano alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa tayari kukaribisha ushirikiano wowote ambao unaleta fursa kwa wateja wake, hivyo shirika litaongeza tija katika utoaji huduma na hivyo kuwarahisishia wateja.

“Tunajisikia fahari sana kuingia katika ushirikiano mwingine na shirika letu la taifa la Reli Tanzania, Wateja wa TRC kwa sasa wataweza kulipia tiketi zao kupitia huduma yetu ya Airtel Money kwa uhuru kabisa” alisema Bi. Beatrice.

Aidha Bi. Beatrice alitoa rai kwa wateja wa Airtel kutumia huduma hiyo ili kuokoa muda na kufanya malipo kwa njia rahisi na salama hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya kwani kwa sasa watakua na uhuru wa kulipia tiketi za usafiri wakiwa mahali popote pale bila kutembelea ofisi za TRC