Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

SHIRIKA LA RELI TANZANIA KUFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI KWA SEKTA BINAFSI


news title here
24
December
2019

Shirika la Reli Tanzania lafungua milango kwa sekta binafsi katika uboreshaji wa mabehewa ili kuendeleza kuimarisha usafiri wa reli nchini Hivi karibuni

Tamko hilo limetolewa na Mh.Waziri Mhandisi Isack Kamwelwe, Waziri wa ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika kikao kifupi na bodi ya wakurugenzi TRC pamoja na menejimenti ya TRC katika ukumbi wa MIKUTANO TRC makao makuu jijini Daresalaam .

Waziri Kamwelwe alielekeza bodi ikae kupanga taratibu sahihi ambazo zitatumika kwa ajili ya ushirikiano huo katika kuendeleza kuboresha sekta ya miundo mbinu nchini na kutatua changamoto ya mabehewa ya mizigo ili kuliwezesha

shirika kutoa huduma kwa ufanisi na kasi.

Waziri Kamwelwe amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya idadi

ya mabehewa ya mizigo ni muda sahihi kuimarisha mikakati iliyoanzishwa ya

kushirikisha wadau katika kukarabati mabehewa ya mizigo ili yaweze kufanya kazi ya kubeba mizigo na kupunguza msongamano wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam ambayo imekuwa ikipokea idadi kubwa ya mizigo kila siku.

Waziri Kamwelwe aliongeza kua mbali na maagizo hayo ameutaka uongozi wa Shirika kuhakikisha inaweka sawa mifumo iliyopo ya ukataji tiketi na malipo ili kuwawezesha abiria kukata tiketi kwa urahisi wanapotaka kusafiri.

Kitendo cha kufungua milango kwa sekta binafsi katika uboreshaji wa behewa ni muendelezo ambao tayari baadhi ya sekta binafsi wanautekeleza kama Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP

limekarabati mabehewa 40 ya mizigo ambayo pamoja na kusafirisha mizigo ya WFP yanatumika kusafirisha mizigo ya wateja wengine.

Pia Shirika linaendelea na mkakati wa kukarabati mabehewa ambapo hivi sasa Shirika linatekeleza mradi wa ukarabati wa mabehewa 200 ya mizigo.

Waziri Kamwelwe amelipongeza Shirika la reli kwa kuboresha miundombinu

ambayo imekuwa ni chachu ya kukuza uchumi wa Shirika na kupelekea kuongeza idadi ya abiria hasa kwa safari za bara na kaskazini na kuwataka kuhakikisha Shirika linarudisha Mali na

majengo yote ya reli nchi nzima yanayomilikiwa nje ya utaratibu.

Waziri aliongeza kuwa Ninawapongeza kwamba mnaenda vizuri

nimesikia Mbeya, Musoma mmesharudisha” hali hii inaonesha Shirika linafanya kazi nzuri kwani kumekuwa na ongezeko la ufanisi katika usafirishaji wa mizigo hususani ya kuelekea Mwanza,

Kigoma na Katavi, sambamba na kurejea kwa huduma za usafiri kutoka Dar es

Salaam kuelekea Moshi na sasa ukarabati unaendelea kutoka Moshi hadi Arusha.

“Pamoja na maboresho ya miundombinu ya reli yanayoendelea, kumetajwa kuongezeka kwa ufanisi kwa kiasi kikubwa katika usafirishaji wa mizigo kwenda

mikoa ya bara hususani Kigoma, Mwanza na Katavi, nawapongeza sana Bodi na Menejimenti kwa jitihada hizi” alisema Waziri Kamwelwe.