Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SGR TANZANIA KUWA KIVUTIO KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA BARANI AFRIKA


news title here
24
June
2023

Mradi wa ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa(SGR),unaoendelea nchini Tanzania kuwa kivutio kwa Nchi mbalimbali barani Afrika zilizoshiriki katika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma yaliyofanyika Victoria Falls, Zimbabwe kwa mara ya tisa tangu kuasisiwa. Maonesho yameanza tarehe 21 Juni hadi 23, 2023.

Shirika la Reli Tanzania(TRC) ni miongoni mwa taasisi ya serikali iliyofanikisha ushiriki katika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika. Maonesho haya yamebeba dhima chini ya kauli mbiu kuu isemayo ”Eneo Huru la Biashara katika Bara la Afrika litahitaji Utawala wa Umma wenye nia madhubuti ili kufanikiwa” (The African continental Free Trade Area Will Require a Fit for purpose African Public Administration to Sucseed).

Tofauti na kauli mbiu kuu maadhimisho yameambatana na kauli mbiu ndogo ambazo ni Diplomasia iliyoimarika, kuoanisha mifumo ya sheria na ushirikiano wa kikanda , kuzuia uhalifu unaovuka mipaka kwa usimamizi mzuri wa uratibu na utekelezaji wa mamlaka ya eneo huru la biashara Afrika, Utawala wa umma uliostawi na kutengeneza mazingira wezeshi ya uwekezaji katika viwanda vya kuongeza thamani ili kuongeza faida za muundo wa eneo huru la biashara Afrika. Kuanzisha teknolojia mpya na muhimu katika usimamizi, ufundi, ujuzi wa kijasiliamali ili kuhakikisha matumizi mazuri ya rasilimaliwatu, fedha na nguvu kazi kupata matokeo chanya ya biashara za kuvuka mipaka. Hizi zote ni miongoni mwa mada zilizojadiliwa katika mkutano wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika,Victoria Falls, Zimbabwe .

Kutokana na teknolojia mpya ya uwekezaji inayoendelea Nchini Tanzania katika kuimarisha sekta ya miundombinu ya reli kwa ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa ( SGR) imekua kivutio kwa washiriki wa maonesho ya maadhimisho kwa kuwa uwekazaji huu utaleta matokeo chanya katika biashara za kuvuka mipaka kwa nchi mbalimbali za Afrika.

Kupitia sera ya taifa na mkakati wa nchi kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 ni Dhahiri kwa taifa kuwa na miundombinu imara na yenye ufanisi kwa kutumia teknolojia mpya ya SGR itachochea utoaji wa huduma bora ya usafirishaji kwa haraka na kwa bei nafuu.

Ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa (SGR) ni nguzo kubwa katika kuchochea na kupunguza gharama na muda wa safari kwa abiria na mizigo. Mataifa yenye nguvu duniani yamejengwa nakujikita katika kuwa na miundombinu imara kwenye utoaji wa huduma za usafiri kwa haraka kutoka mji mmoja hadi mwingine.

Tanzania ni kati ya nchi chache ambazo ni mlango wa nchi zingine katika kupitisha bidhaa kwenda na kutoka, hii ni fursa kubwa kwa taifa kuwekeza kwenye miundombinu imara ya usafirishaji kwa wakati, salama na kwa bei nafuu na dhima hii imekua kivutio zaidi kwa maonesho yanayoendelea Victoria Falls, nchini Zimbabwe.

Wataalamu wa mambo ya usafirishaji duniani wanasema usafiri wa reli hupunguza gharama ya bidhaa kwa asilimia kati 30% hadi 40% na huwa nikichocheo kikubwa cha uchumi,kuwekeza katika ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa Tanzania.

Awamu ya kwanza ya Ujenzi wa SGR ni Dar es Salaam – Mwanza na itaunganisha mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma (makao makuu), Singida, Tabora, Shinyanga, Mwanza na Nchi za maziwa makuu Kama Uganda, Rwanda, Kongo na Burundi. Biashara za kuvuka mipaka kwa nchi mbalimbali imekua dhima kuu katika majadiliano kipindi cha mkutano wa maadhimisho ya wiki ya utumishi barani Afrika.

Kwa awamu ya pili ya ujenzi wa reli yenye kiwango cha kiataifa (SGR) unaendelea Tabora – Kigoma, na baadae kwa kuwa usanifu wa awali umeshafanyika Kaliua – Mpanda – Karema ili kuunganisha na ziwa Tanganyika pamoja na nchi za Kongo, Burundi na Rwanda unaendelea. Kupitia maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa nchini Tanzania imekua kivutio zaidi katika maonesho ya wiki ya utumishi wa umma nchini Zimbabwe.

Muwakilishi Mkuu katika maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa umma barani Afrika kutoka Tanzania ni Mh. Naibu Waziri Ofisi ya Raisi, Menejimenti na utawala bora Mh. Ridhiwani Jakaya Kikweta,alipata fursa ya kuchangia katika kikao cha maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma barani Afrika kipindi cha majadiliano kuhusu maendeleo ya biashara huru kwa nchi za Afrika lakini pia alielezea uboreshaji wa miundombinu, ikiwemo reli, barabara majengo pamoja na kuhakikisha utumishi wa umma unakua bora na wenye tija ili kufikisha malengo katika bara la Afrika.

Mh. Naibu Waziri aliongeza kuwa miundombinu mbalimbali imeweza kufanyiwa kazi nchini Tanzania kwa kuanza na ujenzi wa reli yenye kiwango cha kimataifa (SGR) katika kuwezesha mawasilianiano kutoka Nchi moja kwenda Nchi nyingine zenye maziwa makuu. Reli hii itapokamilika itawezesha nchi kama Uganda,Rwanda,kongo na Burundi kuwafikia kirahisi na kufikishiwa mizigo kwa gaharama nafuu,haraka kwa wakati na salama lakini pia Nchi jirani zitaendelea kujifunza teknolojia hii mpya ya ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) nchini Tanzania kwa kuwa viongozi wa Nchi mbalimbali za Afrika kama Uganda, Zambia na Kongo tayari wameshakuja kujifunza na kushuhudia uwekezaji wa SGR.

Kwa sasa Tanzania iko katika mchakato wa kujenga chuo kitachokua kinatoa Elimu ya teknolojia hii mpya ya reli ya SGR ili kuendeleza rasilimali watu ambao watakua na uwezo wa kujenga, kuendesha na kufanya maboresho endapo kutakua na changamoto.Mh. naibu Waziri aliendelea kusisitiza kuendelea kuimarisha Diploasia ya uchumi kwa Nchi za Afrika, Umoja na ushirikiano.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani Afrika yamefika kilele 23 Juni 2023. Ushiriki wa Tanzania katika maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma barani Afrika kunasaidia kujipambanua kidiplomasia katika Utawala Bora na utekelezaji wa maadhimio yatakayokubaliwa utasaidia Tanzania kuchangia ufikiwaji wa maono ya kuwa na Eneo Huru la Biashara katika Bara la Afrika.