Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SGR NA MGR KUTEGEMEANA KATIKA USAFIRISHAJI WA MIZIGO DAR – KIGOMA


news title here
17
February
2024

Bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania TRC imekagua karakana kuu ya ukarabati wa vichwa vya treni mkoani Morogoro, Februari 16, 2024.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo mwenyekiti wa bodi ya TRC Bw. Ally Karavina ameeleza kuwa ziara hiyo imelenga kufuatilia maendeleo ya ukarabati wa vichwa vya treni ambayo ni shughuli muhimu kwa katika kuhakikisha uhakika wa vifaa vya uendeshaji katika reli ya kiwango cha MGR.

Aidha Karavina meeleza kuwa TRC ina mpango wa kuhakikisha uendeshaji wa SGR na MGR unategemeana kwa upande wa huduma ya treni za mizigo ambapo itasaidia kupunguza muda wa kusafirisha mizigo kutoka Bandari ya Dar Es salaam kuelekea nchi Jirani zinazotumia bandari hiyo.

“Tunataka tutgumie sehemu ya reli ya Kiwango cha SGR iliyokamilika kutengeneza pesa, tutakuwa tunasafirisha mizigo kutoka Dar es Salaam kwa SGR mpaka pale reli hiyo itakapoweza kufika, na kuanzia hapo tutauhamishia mzigo huo katika reli ya MGR ili kuufikisha Kigoma” alisema Bw. Karavina.

Katika kuhakikisha hilo linawezekana, karakana ya ukarabati wa vichwa vya treni Morogoro ni sehemu muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa vichwa vya treni ya MGR vya kutosha.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa TRC Bi. Amina Lumuli amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa karakana ya Morogoro na nyingine, shirika lina mpango wa kuzikarabati karakana zote na kuweka vitendea kazi vya kisasa ili kuleta ufanisi zaidi.

Bi. Amina amesema kuwa “Kupitia mkataba wa ujenzi wa SGR kipande cha Dar ES Salaam hadi Morogoro, tuna mpango mkubwa wa ukarabati wa karakana hii ya Morogoro Pamoja na tawi la Chuo cha Teknolojia ya Reli hapa Morogoro, ili kuhakikisha uendeshaji wa reli hii ya zamani unasaidiana na SGR katika usafirishaji wa mizigo”

Ujenzi wa reli ya kiwango cha SGR kwa vipande vya Dar Es salaam – Morogoro na Morogoro – Makutupora umefikia hatua za umaliziaji huku majaribio ya vifaa vya uendeshaji yakiendelea kati ya Dar Es salaam na Morogoro ambapo inatarajiwa hadi kufikia mwezi julai, 2024 safari za treni za abiria kupitia reli hiyo zianze kati ya Dar Es salaam na Dodoma.