SGR KUA MFANO KATIKA KONGAMANO LA KUKUZA MUSTAKABADHI ENDELEVU WA KUHIFADHI MAZINGIRA

February
2024
Shirika la Reli Tanzania – TRC limeshiriki katika kongamano na mradi wa ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kuwa mfano bora katika kukuza mustakabadhi endelevu wa kutunza mazingira, kongamano limeandaliwa na Benki ya Standard Chartered Tanzania lililofanyika katika hoteli ya Hayyat jijini Dar es Salaam Februari 16, 2024.
Kamishina wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Ndugu Rished Bade alisema kuwa kongamano lina lengo la kuleta uelewa katika kuelimisha watu juu ya umuhimu wa kutunza mazingira na fursa zinazopatikana katika pande mbili za sekta binafsi na Serikali katika kutekeleza miradi ambayo inajali kuhusu mazingira.
“Benki ya Standard Chartered Tanzania iko mbele kwa kutunza mazingira na kutoa mikopo kwenye miradi ambayo ni endelevu na inajali mazingira” alisema Ndugu Bade.
Mkurugenzi Mkuu kutoka TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa alisema kuwa Benki ya Standard Chartered Tanzania inatoa ushirikiano mzuri kwa TRC hivyo kupitia kongamano hili linagusa mradi mkubwa wa kimkakati wa reli yenye kiwango cha kimataifa – SGR ambayo inakumbatia mazingira.
“Mwaka 2020 Benki ya Standard Chartered Tanzania iliweza kutufadhili kwa kiasi cha fedha Dolla Bilioni 1.6, tunafanya nao kazi kwa karibu sana hasa katika kuhifadhi mazingira” alisema Ndugu Kadogosa.
Pia Ndugu Kadogosa alieleza kuwa SGR ni mradi ambao umewekeza kwa kiasi kikubwa katika kuhifadhi mazingira kwa kutumia umeme ambao ni Hydro Gass ambayo ni rafiki kwa mazingira, pia katika njia ya reli kumeoteshwa majani pembezoni mwa reli na kwenye milima ambayo mahandaki yamepita, mkandarasi amechoronga chini zaidi kuepuka ukataji miti.
”TRC imekua mfano wa kuigwa kwa Afrika nzima kwakua na mradi mkubwa ambao unakumbatia mazingira na kuweka mazingira mazuri kwenye jamii” alisema Ndugu Kadogosa.
Mabadiliko ya tabia nchi huathiri maisha ya watu hivyo ni vyema kujua jinsi ya kujilinda na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi kama ukataji miti na uchomaji wa misitu kiholela ili kuweza kujilinda.
Mpaka sasa mradi wa Ujenzi wa ujenzi wa Reli ya kiwango cha Kimataifa(SGR) kwa awamu ya kwanza Katika kipande cha kwanza Daressalaam -Morogoro umefikia asilimia za ujenzi 98.84, kipande cha pili Morogoro - Makutopola 96.35%, Makutopola -Tabora 13.86%, Tabora -Isaka 5.38% ,Isaka-Mwanza 52.69%