Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SERIKALI YA TANZANIA NA BENKI YA STANDARD CHARTERED ZAWEKEANA SAINI MKOPO WA UJENZI WA RELI YA KISASA – SGR


news title here
13
February
2020

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na Mipango yatiliana saini makubaliano ya Mkopo wa Shilingi Trilioni 3.3 za kitanzania kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa reli ya Kisasa – SGR Daresalaam-Makutupora, Singida, katika ukumbi wa Benki Kuu jijini Dar es Salaam Februari, 13, 2020.

Mkataba huo ni kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ambapo wabia wapatao 17 ikiwemo Serikali ya Denmark na Sweden kutoka Ulaya wakishirikiana na Benki ya ‘Standard Chartered’ ambaye ni mratibu wa mkopo huo wametoa mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR kuanzia Morogoro – Makutupora mkoani Singida.

Kwa niaba ya Serikali Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani wameweka saini katika makubaliano hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yatasaidia kuongeza nguvu katika utekelezaji wa mradi huo uliofikia zaidi ya 25% kwa kipande cha Morogoro – Makutupora, Serikali ya Tanzania imesimamia mradi huo kwa fedha za ndani tangu kuanza kwake mwaka 2018.

Aidha Dkt. Mpango amesema kuwa Benki ya Standard Chartered na washirika wake wameonesha nia kuchangia katika Mradi mikubwa ya kimkakati kwa sababu tangu Serikali ilipotangaza kuyaomba mabenki ya ndani na nje ya nchi kujitokeza kuchangia katika miradi mikubwa yenye vipaumbele kwa taifa ili kufikia malengo ya taifa baadhi yao walikataa hivyo ameishukuru benki hii kwa kuratibu zoezi hili

“Mradi huu wa kujenga reli ya kisasa ni mradi ambao unakwenda kubadilisha maisha ya watanzania, hivi sasa tayari umewaajiri watanzania zaidi ya ya 14000, mradi huu unatumia baadhi ya malighafi na vifaa ambavyo vinazalishwa hapa nchini hususani saruji, mchanga lakini nguvu kazi ni vijana wetu”. alisema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango ameongeza kuwa deni la nchi yetu bado ni himilivu na ni lazima tukope kwa sababu reli hii tunawekeza takribani miaka 200 ijayo. Hii reli iliyopo (ya zamani) ina takribani miaka 100, hii ya kisasa itakaa zaidi ya miaka 200. Pia amesisitiza kuwa Serikali itasimamia fedha hizo kuhakikisha zinatumika kama ilivyopangwa.

“Mkopo huu tunachukua na tutaulipa miaka 20 kwa hiyo muda tunao, nawashukuru wabia hawa ambao wameunga mkono jitihada za Serikali za kubadilisha uchumi wa nchi kwa kutupatia mkopo huu wa Shilingi Trilioni 3.3”. alisema Dkt. Mpango

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Bw. Sanjay Rughani amesema kuwa zoezi la kuwekeana saini ya makubaliano ya mkopo kwa ajili ya mradi wa reli ya kisasa ni hatua kubwa hasa katika suala la uchumi pamoja na upande wa uwekezaji.

“Afrika inabaki kuwa kipaumbele kwa biashara yetu na wateja kwa ujumla, tunajivunia kutumia utaalamu wetu kusaidia serikali ya Tanzania na fedha zinazohitajika kwenye mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa wa SGR”. alisema Bw. Sanjay.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amesema kuwa kupatikanaji wa mkopo kwa ajili ya mradi huo, kutaongeza kasi ya ujenzi huo kwani mpaka sasa ujenzi kutoka Dar es Salaam mpaka mkoani Morogoro umefikia asilimia 73, hivyo mkopo huo utawezesha ujenzi wa reli hiyo kutoka mkoani Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida.