Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​SEKRETARIETI YA BARAZA LA USALAMA LA TAIFA YAIPONGEZA TRC KWA KASI YA UJENZI WA RELI YA KISASA - SGR


news title here
29
March
2019

Sekretarieti ya Baraza la Usalama la Taifa yafanya ziara kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR Dar es Salaam - Makutupora Machi 2019.

Katika ziara hiyo iliyofanyika kuanzia Dar es Salaam katika eneo ambalo stesheni kubwa ya kisasa ya treni za umeme itakayoungana na daraja refu la kilometa 2.6 hadi Kilosa mkoani Morogoro, wajumbe walipata fursa ya kuona kasi ya mradi pamoja na kujifunza kuhusu hatua tofauti za ujenzi wa reli.

Aidha waratibu wasaidizi wa Baraza wakiongozwa na Mratibu msaidizi Mkuu wa Sekretarieti ya Baraza la Usalama la Taifa Brigedia Jenerali Masile Machanga wamefurahishwa na kasi ya ujenzi na kusema kuwa ni vigumu kwa wananchi kuelewa kinachofanyika katika mradi huo lakini kazi ni kubwa na inaonekana mbali ya kuwepo changamoto kadhaa katika mradi ikiwemo hali ya hewa.

Mratibu msaidizi Mkuu wa Sekretarieti ya Baraza la Usalama la Taifa Brigedia Jenerali Masile Machanga amesema kuwa pamoja na mambo mengine kazi yao kubwa ni kuishauri Serikali namna ya kufanya ili miradi mikubwa ya Kitaifa imalizike kwa wakati lakini pia wameshuhudia namna nchi ya Viwanda na uchumi wa kati inawezekana Tanzania.

Amesema Brigedia Jenerali Masile “Kitu kingine ambacho tumekiona ni Ushahidi tosha kwamba sasa nchi yetu inatoka katika ulimwengu wa tatu kwenda ulimwengu wa kati kwa sababu reli kama hii ilikuwa inaonekana Ulaya lakini leo tunaiona nyumbani Tanzania hiyo ni ishara kwamba nchi ya viwanda na uchumi wa kati inawezekana”