Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA WA UJENZI WA RELI YA KISASA MAKUTUPORA - TABORA


news title here
28
December
2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGRkipande cha Tatu Makutupora – Tabora chenyeurefu wa kilomita 368 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam Disemba 28 , 2021.

Mkataba huo umesainiwa kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania – TRC Ndugu Masanja Kadogosa kwa niaba ya Serikali na Kaimu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Merkezi Bwana Erdem Arioglu

Mhe. Raisi Samia ameeleza kuwa Mkataba wa Ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Tatu Makutupora - Tabora utagharimu kiasi cha shilingi za kitanziania Trillion 4.406 ambapo mpaka sasajumla ya fedha ambazo serikaliimewekezakatika ujenziwa Reli ya SGRkwa awamu ya kwanza Dar es Salaam - Mwanza kwa vipande vinne kati ya vitano yani Dar es Salaam –Morogoro, Morogoro - Makutupora, Makutupora - Tabora na Mwanza - Isaka imefikia shilingi za Kitanzania Trilioni 14.7 ukijumlisha na kodi ya ongezeko la thamani (VAT).

“Mkataba huu ni wenye thamani za kitanzania kama ilivyosemwa Trilioni 4.41 pamoja na kodi ya ongezeko la thamani sasa inafanya jumla ya uwekezaji ya vipande vinne kati ya vitano vinavyoendelea au vya awamu ya kwanza vya Reli kwa ajili ya ujenzi wa kutoka Dar Es Salaam – Mwanza kufikia kiasi cha Shilingi Trilioni 14.7 za kitanzania na hizi ukijumlisha na kodi.”Alisema Mheshimiwa Raisi Mama Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Rais Samia ameipongeza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na Shirika la Reli kwa usimamizi mzuri wa mradi licha ya uwepo wa changamoto za UVIKO19 pamoja na mvua kubwa zilizonyeshwa mwaka 2020

“Nachukua fursa hii pia kuipongeza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi , Bodi ya Manejimenti na Wafanyakazi wa TRC kwa juhudi zote mnazozifanya katika kuendelea kusimamia ujenzi wa mradi huu mkubwa wa kimkakati unaondelea wa ujenzi wa SGR ninafahamu kuwa ujenzi huo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO19 na mvua zilizonyesha mwaka jana” alisema Mhe. Rais

Mheshimiwa Rais ameeleza kuwa mchakato waujenzi wa kipande cha nne Tabora – Isaka na ujenzi wa awamu ya pili Tabora – Kigoma upo mbioni na ameliagiza Shirika la Reli Tanzania chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kukamilisha taratibu za manunuzi za kumpata wakandarasi watakaojenga vipande hivyo.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa kutokana na kuimarika kwa uchumi wa nchi, kutoka uchumi wa chini kwenda uchumi wa kati pamoja na kukua kwa viwanda nchini, sekta ya uchukuzi ni muhimu na kwa kulitambua hilo ujenzi wa reli ya kisasa utaleta chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kuelekea uchumi ulio bora.

“Sote tunafahamu kuwa sekta ya uchumi ni muhimu sana kwa Taifa kwa ujumla, sekta hii ndio chachu kuu ya kuwezesha nchi yetu kufika lengo la viwanda na Uchumi wa kati” alisema Prof. Mbarawa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Reli Tanzania Ndugu Masanaja Kungu kadogosa ameeleza kuwa ujenzi wa reli Kipande cha tatuchenye Kilomita 368 ambapo urefu wa njia kuu ni Kilomita 294 na njia za kupishana ni Kilomita 74 utagharimu Serikali takribani Shilingi za Kitanzania Trilioni 4.406 utachukua miezi arobaini na sita (46) hadi kukamilika kwake na matarajio ni kukamilikani mwezi Oktoba, 2025.

Pia Mkurugenzi Mkuu TRC ameongeza kuwa Mkataba wa ujenzi wa reli kipande cha tatu ni mkataba ambao hautaathiriwa na mabadiliko ya kupanda au kushuka kwa bei za bidhaa za ujenzi (Fixed contract) sokoni kama vile saruji, nondona chuma lengo kuu likiwa ni kuiletea nchi faida na kuokoa fedha kama ilivyofanyika katika ujenzi wa kipande cha kwanza na cha pili ambapo serikali iliokoa zaidi ya Shilingi za Kitanzania Trilioni1.4.

Hafla ya utiaji saini viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Hussein Katanga, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Mawaziri, Naibu Mawaziri, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makala, Wakuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC Prof. John Kondoro, Watendaji wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wawakilishi kutoka kampuni ya Yapi Marekezi, Wenyeviti wa Kamati za Bunge, Uongozi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Menejimenti ya TRC.