Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

RAIS MAGUFULI NA RAIS MUSEVENI WATEMBELEA BANDA LA TRC


news title here
06
September
2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Rais Kaguta Museveni wa Uganda watembelea banda la Shirika la Reli Tanzania - TRC katika ufunguzi wa kongamano la kwanza la Biashara kati ya Tanzania na Uganda linalofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha J.K Nyerere jijini Dar es Salam Septemba 6, 2019.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Rais Kaguta Museveni wa Uganda walitembelea Mabanda yaliyoshiriki Kongamano hilo ambapo walitembelea Banda la Shirika la Reli Tanzania na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa kuhusu Miradi na Huduma zitolewazo hususani Huduma ya usafirishaji Mizigo kutoka Dar es Salaam hadi Kampala nchini Uganda kupitia ziwa Victoria.

Mkutano huo wenye lengo la kufungua fursa za kibiashara pamoja na kuimarisha ushirikiano unahudhuriwa na Viongozi wa Serikali kutoka Tanzania na Uganda wakiwemo Mawaziri na Naibu Mawaziri, Wafanyabiashara, Wakuu wa Mikoa, Mabalozi, Wawakilishi wa Jumuiya ya Wafanyabiasha Tanzania na Uganda, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Taasisi na Mashirika ya Serikali pamoja na Wawekezaji kutoka Tanzania, Uganda na nchi nyingine.

Kongamano litaleta tija katika kuimarisha sekta ya Viwanda, Kilimo, Biashara na Usafirishaji kwa kuitumia vyema miundombinu ya Biashara kati ya Tanzania na Uganda ikiwa ni mwaka mmoja Tangu kufunguliwa kwa njia ya Usafirishaji wa Mizigo kati ya Tanzania na Uganda kwa kutumia Reli kupitia Ziwa Victoria ambapo zaidi ya Tani 36,000 za Mizigo zimesafirishwa kwa kipindi hicho.