Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

JESHI LA POLISI LAHAMASIKA KUIMARISHA HALI YA USALAMA KATIKA MAENEO YALIYOPITIWA NA MRADI WA SGR


news title here
28
February
2019

Mkuu wa Jeshi la Polisi Kamanda Simon Sirro atembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR Dar es Salaam hadi Kilosa kuona hali ya usalama wa mali na wafanyakazi katika mradi wa SGR hivi karibuni Februari 2019.

Kamanda Simon Sirro amesisitiza kuwa suala la usalama katika mradi wa SGR ni la msingi hivyo kuna ulazima wa jeshi la polisi kujipanga ili kuhakikisha usalama unakuwa wa kudumu katika maeneo ya mradi wakati wa ujenzi na pindi mradi utakapokamilika

Alisema Kadogosa, “Ugeni wa Kamanda Sirro una maana kubwa kwa TRC na taifa kwa ujumla kwa kuwa ni mradi unaoendelea, huu ni mradi mkubwa wa kitaifa na kuna manufaa makubwa ya kitaifa kuona kwamba mradi unamalizika kwa muda lakini uwepo wa usalama kwa wafanyakazi kwa kuwa tunafanyakazi saa 24”

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania limeendesha oparesheni kadhaa kudhibiti wahalifu wakiwemo wezi wa mafuta katika kambi za mradi za Soga na Ngererengere, aidha Shirika linaendelea kushirikiana na jeshi kupitia kikosi cha Polisi Reli kuhakikisha ulinzi na usalama maeneo ya mradi.