Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

RAIS MAGUFULI AZINDUA AWAMU YA PILI YA UJENZI WA RELI YA KISASA KUTOKA MORODORO HADI MAKUTUPORA MKOANI DODOMA


news title here
21
May
2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aweka jiwe la msingi awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) yenye urefu wa 426km kutoka Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma, hatua hiyo itaifanya Tanzania kuwa na treni ya umeme itakayokwenda kwa kasi ya 160 kwa saa kwa treni ya abiria na 120 kwa saa kwa treni ya mizigo.

Akihutubia mjini Dodoma kabla ya kuweka jiwe la msingi, Rais Magufuli amesema kumalizika kwa ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) itasaidia kutoa ajira 30,000 za moja kwa moja na ajira 60,000 zisizo za moja kwa moja. "Reli ya Kisasa na Banadari kavu itakayojengwa mjini Dodoma itasaidia kuleta maendeleo kwenye mikoa ya kati" alisema Rais Magufuli, pia aliongeza kuwa baada ya ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hado Dodoma serikali itaendleza ujenzi huo hadi mkoani Mwanza kukamilisha km1.219.

Reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma yenye urefu wa km522 inajengwa na kampuni ya kituruki ya Yapi Markez. Ujenzi wa reli hii ya kisasa utasaidia usafirishaji wa abiria na mizigo kutoka na kwenda nchi za jirani za Uganda, Zambia, the Democratic Republic of the Congo, Burundi na Rwanda.

Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema kuwa reli hii itakuwa na uwezo wa kusafirisha Tani 10,000 za mizigo kwa mara moja. "Tunapoteza wateja kwenye bandari ya Dar es Salaam kutokana na kutokuwa na miundombinu ya kuaminika, lakini baada ya mradi huu tutaweza kuwarudisha wateja hao" alisema Waziri Mbarawa

Awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutupora mkoani Dodoma unatarajiwa kukamilika November 2020.