Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATEMBELEA KUONA UJENZI WA RELI KISASA


news title here
09
May
2018

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa atembelea ujenzi wa reli ya kisasa(SGR) na kukagua ujenzi wa tuta na kiwanda cha kutengeneza mataruma ya zege na kumtaka mkandarasi Yapi Markes na Motaengel Africa anayejenga reli hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro kilomita 205 kuhakikisha ujenzi unakamilika ndani ya wakati.
"Hakikisheni kazi ya ujenzi wa tuta na kiwanda cha kutengeneza mataruma ya zege vinakamilika katika muda wa mitatu kutoka sasa ili kwenda na ratiba ya ujenzi huu" alisem Prof. Mbarawa
Akizungumza mara baada ya kukagua tuta litakapojengwa reli hiyo kutoka Pugu, Soga hadi Ngerengere Profesa mbarawa amepongeza kazi inayoendelea na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi ili kazi ya kutandika reli ianze katika muda mfupi ujao.
Aidha Profesa Mbarawa amemuagiza mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Ndg. Masanja Kadogosa kuanza mchakato wa kuagiza vichwa vipya vya treni vinavyowiana na reli hiyo ili itakapokamilika visiwe na hoja ya kusubiri vichwa hivyo.
Pia amesisitiza umuhimu wa Shirika la Reli Tanzania kuandaa wataalamu watakaotumika kuendesha reli hiyo ya kisasa kwa kuwapatia mafunzo ya kiufundi na kibiashara ili kuhakikisha utendaji wa reli hiyo unakuwa wenye tija.
Ujenzi wa reli ya kisasa(Standard Gauge Railway) awamu ya kwanza inayoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro yenye urefu wa Kilomita 205 unatarajiwa kukamilika mwaka 2019.
Zaidi ya kilomita 2600 za reli ya kisasa zinatarajiwa kujengwa kutoka Dar es Salaam-Morogoro-Isaka-Mwanza na Tabora ili kuiunganisha Tanzania na nchi za jirani kwa lengo la kuboresha mahusiano ya kiuchumi.