Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

MSEMAJI MKUU WA SERIKALI Dk. HASSAN ABBASI AIPONGEZA TRC KWA KUTANGAZA VYEMA MIRADI NA HUDUMA ZITOLEWAZO NA TRC.


news title here
22
August
2019

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassan Abbasi ametembelea ofisi ya makao makuu Shirika la Reli Tanzania - TRC kwa lengo la kutoa elimu kuhusu muongozo na Mkakati wa Mawasiliano ya Shirika pamoja na kujionea maendeleo ya ujenzi wa stesheni ya reli ya kisasa – SGR jijini Dar es Salaam Agosti hivi karibuni, 2019.

Katika Warsha hiyo fupi Msemaji Mkuu wa Serikali alipata fursa ya kuelezea miongozo ya mawasiliano ndani ya shirika na nje ya shirika kwa kuwa upo umuhimu wa kuweka miongozo juu ya nani wa kuzungumza, nini cha kuzungumza na kwa wakati gani.

Pia ili kuhakikisha mawasiliano na habari vinakwenda sambamba Msemaji Mkuu amesisitiza suala la ushirikiano kati ya Idara na Vitengo ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa umma kwa wakati.

Dkt. Abbasi amekipongeza kitengo cha Habari na Uhusiano TRC kwa kazi kubwa ya kutoa habari kwa umma kuhusu maendeleo ya miradi pamoja na huduma zinazotolewa na shirika, pia amesisitiza kitengo cha habari na uhusiano kuendelea kuitangaza miradi ya shirika ili wananchi waweze kuona maendeleo yanayofanywa na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedari Dk.John Pombe Magufuli.

“tunaona kazi kubwa ya kitengo cha Habari na Uhusiano, sio leo ipo siku mtakumbukwa aliongeza Dk. Abbasi "nafurahi, viongozi wanaona na sisi tunaosimamia tunapata mrejesho, hongereni sana”

Aidha, Dkt. Abbasi amebainisha umuhimu wa kutoa habari kwa umma kwa wakati sahihi kwa kuwa Serikali imewekeza pesa nyingi za wananchi katika Miradi na namna pekee ya kuujulisha umma matumizi ya pesa hizo ni kupitia habari na mawasiliano ya kimkakati kwa umma. “kuisemea serikali na kuitangaza miradi ya serikali ni kitu kikubwa sana na muhimu kwa serikali na taasisi” alisema Dkt. Abbasi

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amemshukuru Dkt. Abbasi kwa Warsha fupi ya muongozo na mkakati wa mawasiliano utakaoliwezesha shirika kutoa taarifa kwa utaratibu mzuri bila kuwepo athari kwa shirika na umma kwa kuepuka upotoshaji wa taarifa muhimu, Mkurugenzi pia amewataka wakuu wa Idara na Vitengo kufuata muongozo huo katika mawasiliano ya kila siku kwa kushirikiana na kitengo cha Habari na Uhusiano ili kuleta ufanisi katika mawasiliano.

“Suala la ‘’ sio suala tu la kuzungumza, bali ina maana kubwa kwenye taasisi na katika taifa” alisema Kadogosa