Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​MKURUGENZI MKUU TRC AFUNGUA WIKI YA SHIRIKA LA RELI TANZANIA LEO KWA KUFANYA MKUTANO NA WAANDISHI HABARI


news title here
12
December
2019

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania – TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amezungumza na Waandishi wa Habari wakati wa ufunguzi wa wiki ya TRC na kuelezea Miaka minne ya Uongozi wa Mh.Rais Dkt.John Pombe Magufuli na mapinduzi yaliyofanyika katika sekta ya reli nchini Leo tarehe 12.12.2019 katika Ukumbi wa mkutano Habari maelezo JICCC Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu ameelezea kuhusu utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Serikali ambayo Shirika la Reli limepewa dhamana ya usimamizi, uendeshaji pamoja na utekelezaji ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa –SGR, Mikakati ya ujenzi wa Reli ya Kisasa Mwanza – Isaka, uboreshaji wa Reli ya Kati Dar es salaam – Isaka, uboreshaji wa mabehewa sambamba na kurejea kwa huduma za usafiri wa treni Dar es Salaam – Kampala na Dar es Salaam – Moshi.

Mkurugenzi mkuu amepata fursa ya kueleza mafanikio mengi ambayo Shirika limepata ndani ya miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano hususani katika uendeshaji Shirika na utekelezaji wa miradi ya kitaifa katika sekta ya miundombinu ya reli nchni.

Mafanikio hayo aliyanzungumza kwa upande wa miradi miwili ya ujenzi wa reli ya kisasa na uboreshaji wa reli ya kati sambamba na urejeshaji wa treni za mizigo nchini Uganda sanjali na urejeshaji wa treni ya abiria na mizigo mkoani.

Aidha alifafanua kuwa moja ya mafanikio makubwa ambayo Serikali imefanya ni kuziunganisha kampuni mbili ambazo ni kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli – RAHCO na Kampuni ya Reli Tanzania – TRL na kuunda Shirika la Reli Tanzanzia – TRC tutokana na kuunganika kwa makampuni hayo kumewezesha kuongeza ufanisi katika uendeshaji na utendaji kazi ndani ya Shirika sambamba na kuongeza pato kwa mwaka 2018 /19 kufikia TSh. 30,041,773,815/=.

Ndugu kadogosa alitumia mkutano huo kuwaeleza wandishi kuhusu urejeshaji wa treni ya mizingo kutoka Dar es Salaam mpaka nchini Uganda kwa kupitia ziwa Victoria ambapo kwa miaka miwili Shirika limesafirisha jumla ya tani 52,709. kupitia usafirishaji wa mizingo kutoka nje ya nchi kumejenga uhusiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Uganda hivyo kuleta maendeleo na kukuza uchumi nchini. Lakini pia kwa upande wa urejeshaji wa huduma ya treni Tanga – Moshi mwaka 2018 Shirika limesafirisha jumla ya tani 4800 kwa muda wa miezi 6.

Hata hivyo Mkurugenzi amegusia juu ya huduma ya usafiri wa abiria kutoka Dar es Salaam mpaka Moshi ambazo zimeanza mwezi huu ambapo Shirika limepokea maombi kutoka kwa wateja wakiomba kuongezewa siku za safari ambazo zilkuwa safari 4 na Shirika kuamua kuongeza safari 6 kwa wiki.

“Hata hivyo bado kuna mafanikio katika reli ya kati ambapo jumla ya tani 1,456,537 katika reli ya kati zimesafilishwa na kwa upande wa treni za abiria mikoani jumla ya abria 578,439 wameongezeka kwa mwaka 2018¬/19” Hayo yamebainishwa na Mkrugenzi Mkuu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.

Katika hatua nyingine Mkurungenzi Mkuu alinzungumza kuhusu wa Mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa – SGR na uboreshaji wa reli ya kati ambapo alielezea maendeleo ya ujenzi, ubora wa reli ya kisasa sambamba na faida zinazopatikana katika mradi na baada ya mradi kukamilika. Alibainisha Moja ya ubora wa reli kisasa ni upande wa mwendokasi na uwezo wa kubeba mzigo mkubwa hasa kwa nchi ya Congo ambayo inauchimbaji wa madini yenye uzito mkubwa pia teknologia ya mawasiliano katika uendeshaji.

“Niwahakikishie kuwa kinachotofautisha reli yetu na nchi zingine uwezo wa kubeba mzigo na teknolojia ya nawasiliano. Tanzania kuwa na reli yenye mwendokasi wa KM 160 kwa saa na yenye uwezo wa kubeba mizigo na abiria kwa nchi za Afrika ni nchi yetu pekee” Alisema Ndugu Kadogosa.

Aliongezea kuwa reli hii ya kisasa itakuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya viwanda, kilimo na biashara. Reli ya kisasa itachochea sekta hizo kukua kwa usafirishaji na uchukuzi wa uhakika kupitia reli lakini pia kadri zinavyokuwa ndipo ongezeko la uhitaji wa rasilimali watu utakavyoo ongezeka ambapo zitaajiri watu wengi katika shughuli za uzalishaji, kilimo na viwandani, Kwa hiyo reli itapelekea utoaji wa ajira za kutosha katika sekta hizo nyeti na kupelekea uchumi kukua kwa kasi.

Si hivyo tu vile vile SGR imebeba maono makubwa katika sekta ya Kilimo kutokana na kwamba wakulima wengi watafaidika na reli hii katika uzalishaji na usafirishaji wa mazao kutoka eneo la uzalishaji mpaka sokoni ambapo mkulima atatumia muda mchache kusafirisha mazao. Lakini pia ghalama za mazao zitapungua kutokana na kwamba mkulima atakuwa na uwezo wa kusafirisha mazao mengi kwa wakati mchache. Pia kupitia reli ya kisasa itaongeza idadi ya watanzania kujikita katika sekta ya kilimo kwani watakuwa na uhakika wa kusafirisha mazao yao kwa haraka na kwa bei nafuu mpaka sokoni.

“Reli yetu itakapo kamilika itakuwa na mchango mkubwa biashara na viwanda ambapo itapunguza gharama za uzalishaji na usafirishaji ambapo kwa sasa bei ya saruji Mwanza na Dar es Salaam ni tofauti lakini yote ni kwa sababu ya gharama za usafirishaji, reli hii ikikamilika itapunguza gharama za usafirishaji lakini pia ununuzi wa malighafi” Alisema Mkurugenzi Mkuu.

Vile vile Mkurugenzi alieleza kuhusu faida za miradi hii yote inayoendelea nchini kuwa inafaida kwa jamii hata katika wakati huu wa ujenzi ambapo watanzaia 14,000 wamepata ajira za moja kwa moja katika mradi pia wakazi wa maeneo ya mradi wamepata fursa ya kufanya biashara hivyo kupelekea kubadili maisha yao katika swala la kuwaongezea kipato na kukuza uchumi wa nchi.

Mwisho kabisa Mkurugenzi aliwashukuru Wandishi wa habari kwa kuja kutimiza wajibu wao kwa kufikisha habari kwa uuma hasa katika miradi hii mikubwa ambayo ni ya kimkakati na ni moja ya miradi yenye lengo la kuleta mapinduzi katika uchumi wa nchi ifikapo 2025.

Mkurugenzi Mkuu TRC aliongeza kuwa alitoa rai kwa watanzania wote kwa pamoja kuwa walinzi wa miundombinu ya reli kwani ni ya watanzania wote na vizazi vijavyo.