MENEJIMENTI YA TRC YAANZA MAFUNZO YA MFUMO WA UPIMAJI WA UTENDAJI KWA WATUMISHI
.jpg)
August
2021
Shirika la Reli Tanzania - TRC laanza kupokea mafunzo ya siku tatu kuhusu mfumo wawazi wa upimajiwa utendaji kazi wa watumishi – OPRAS(Open Performance Appraisal System), mafunzoambayo yanafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Bandari jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 2 hadi 4, 2021.
Mafunzo yamefunguliwana kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bi. Amina Lumuli ambapo wakuu wa idara na vitengo wa Shirika la Reli wameshiriki katika mafunzo hayo yanayoendelea ili kuleta ufanisi na uwajibikaji katika majukumu ya kila siku ya watumishi wa Shirika.
Mfumo huu ni wa wazi na shirikishi ambapo mwajiriwa na mwajiri wataweza kushirikiana kikamilifu na kuwa na makubaliano ya pamoja ya namna ya kutekeleza mipango ili kutimiza malengo ya Shirika, mfumo huu utasaidia pia katika kujenga mahusiano mazuri kazini, kupata matokea chanya katika utendaji na kurahisisha ufuatiliaji wa ustawi wa watumishi kazini.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu TRC Bi. AminaLumuli amebainisha kuwa mafunzo haya kwa awamu ya kwanza yanatolewa kwa wakuu wa idara na vitengo na baadaye yatatolewa kwa watumishi wa ngazi za chiniili waweze kuutumia mfumo huo katika kuripoti utendaji kazi.
“Tunakwenda kwenye utaratibu wa upimaji wa ufanyaji kazi wa utumishi wa umma ambao ni mfumo wa wazi wa upimaji kazi OPRAS, kwahiyo semina hii ya siku tatu imejumuisha wakuu wa idara na vitengo ili kupata uelewa wa ujazaji wa fomu hizo kwa kutumia malengo ya taasisi, baada ya kupata mafunzo haya mfumo utaanza kutumika rasmi kwa wafanyakazi wote” alisema Bi. Amina Lumuli.
Bi. Amina ameongeza kuwa Shirika limeazimia kubadilisha utamaduni wa ufanyaji kazi ambapo kwa sasashirika linatazamia wafanyakazi kufanya kazi kwa kujipima na kupimana kutokana na majukumu elekeziwaliyopangiwa kulingana nadhima ya shirika.
Paulinus Mbehoma, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo amesema kuwa pindi wafanyakazi watakapoanza kutumia mfumo wa OPRAS itakuwa ni rahisi kila mtumishi kutekeleza majukumu aliyopangiwa na idara yake ili kufikia malengo ya taasisi.
Naye muwezeshaji kutoka Tume ya Utumshi wa Umma Bi. Cornelia Mvula ameleza kuwa lengo kuu la mafunzo haya kwa wafanyakazi wa Shirika la Reli ni kuwawezesha kufahamu jinsi ya utendaji kazi kama watumishi wa umma na pia kupitia mafunzo haya yatajenga uadilifu katika utendaji kazi na kuondoa uonevu, uvivu na uwajibikaji katika taasisi za serikali.