Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA MIUNDOMBINU YA RELI NCHINI


news title here
25
March
2024

Shirika la Reli Tanzania - TRC limefanya mkutano na wahariri pamoja na waandishi wa habari katika jengo la stesheni ya SGR lililopo jijini Dar es Salaam Machi 25, 2024.

Mkutano huo ambao ulilenga kuelezea mapinduzi yaliyofanywa na Serikali ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania katika sekta ya miundombinu ya reli Tanzania na katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mkurugenzi Mkuu TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa alieleza kuwa TRC inaendelea na ukarabati wa njia ya kati kupitia mradi wa 'Tanzania Intermodal and Rail Development Project - TIRP'.

“Mtandao wa reli umegawanyika katika kanda tatu, ambazo ni ukanda ya Kati, ukanda wa Kusini na ukanda wa Kaskazini” alieleza Ndugu Kadogosa.

Vilevile Ndugu Kadogosa alisema kuwa TRC inaendelea na ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR kwa awamu ya kwanza inayojumuisha ujenzi wa mtandao wa reli wenye jumla ya kilomita 1,219 kutoka Dar es Salaam - Mwanza.

“Ujenzi huu wa SGR utakua moja ya nyenzo kubwa katika sekta ya uchukuzi nchini” alieleza Ndugu Kadogosa.

Aidha, Ndugu Kadogosa alieleza kuwa Serikali imekuwa ikiweka msukumo wa kibajeti wa utengaji rasilimali fedha ili kuhakikisha ujenzi wa miundombinu ya reli unatekelezwa na kukamilika kwa wakati.

“Wakati Mhe. Rais anaingia madarakani, kwa upande wa reli alikuwa muwazi na kuahidi kumalizia kipande alichokikuta na kuendeleza vipande vingine” aliongezea Ndugu Kadogosa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano kutoka TRC Bi. Jamila Mbarouk alitoa shukurani kwa wahariri na waandishi wa habari kwa kufikisha taarifa sahihi za miradi inayotekelezwa na TRC pamoja na maendelo yanafanywa na serikali ya awamu ya sita katika sekta ya reli.

“Watu wa tasnia ya habari ni mabalozi sahihi wa kufikisha taarifa kwa umma, TRC inathamini mchango wenu kwa kuweza kuhakikisha taarifa zinafika wakati sahihi kwa umma kwa kudumisha maendeleo ya taifa letu” alisema Bi. Jamila.

Mhariri Mkuu wa Africa Media Group Limited Bi. Esther Zelamula ambaye amewawakilisha wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini alisema kuwa jukumu la wana habari ni kushiriki kikamilifu katika kutangaza mazuri yanayofanywa na Serikali pamoja na Shirika la reli.

“Vyombo vya habari ni mhimili wa nne wa Dola, hivyo vina umuhimu mkubwa kwa umma na hatuna budi kuwa na uzalendo” alisema Bi. Esther.

Hata hivyo TRC linaendelea na ununuzi wa vitendea kazi kwaajili ya uendeshaji na ukarabati wa reli ambavyo umegawanyika katika makundi matano ikiwemo ununuzi wa vichwa vya umeme (Electric Locomotive) 19, Seti za treni ya umeme (Electric Multiple Unit) 10, mabehewa ya abiria 59, mabehewa ya mizigo 1,430 pamoja na mashine na mitambo 24 ya matengenezo ya njia ya SGR.