Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

MAKATIBU WAKUU NA NAIBU WAKAMILISHA ZIARA YAO SGR


news title here
03
March
2020


Makatibu wakuu na Naibu Makatibu wa wizara tofauti nchini wakamilisha ziara ya siku mbili katika Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR Dar es Salaam - Morogoro - Dodoma Machi 03, 2020.

Ziara hiyo iliyofanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia Machi 02 - 03, 2020 kwa kutembelea maeneo ya mradi wa SGR kwa lengo la kuona maendeleo ya mradi na kuona namna watendaji hao wa wizara za serikali wanaweza kushirikiana kuhakikisha mradi huo unakuwa na manufaa wakati wa ujenzi na pindi utakapokamilika.

Makatibu wamekamilisha ziara yao kwa kukagua mradi wa SGR kipande cha kwanza cha Dar es Salaam - Morogoro ambapo walitembelea kambi za SGR za Ngerengere na Soga pamoja na kuona kazi kubwa inayofanyika kwa kipande cha Dar es Salaam - Morogoro ambacho ujenzi wake uko mbioni kukamilika, kikiwa zaidi ya asilimia 75.

Akiongea kwenye Ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Dkt.Leonard Chamuriho amempomgeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kadogosa na Managejimenti ya Shirika pamoja na Mkandarasi Yapi Merkezi kwa Maendeleo mazuri ya Mradi.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amewashukuru Makatibu wakuu na Manaibu kwa kutembelea Mradi na kuona jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano Chini ya Uongozi wa Mhe.Dkt John Pombe Magufuli kwa kujenga Reli hii Ya Kisasa ambayo itakuwa mkombozi wa wananchi hasa katika sekta ya Uchumi na Maendeleo katika jamii .