Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​MACHIFU WAIPA HEKO SERIKALI KUANZA SAFARI ZA TRENI YENYE KIWANGO CHA KIMATAIFA


news title here
21
July
2024

Shirika la Reli Tanzania - TRC limepokea ugeni wa Machifu wa makabila mbalimbali Tanzania katika stesheni kuu ya SGR ya Dodoma Julai 20, 2024.

Machifu wamefanya ziara fupi ya kutembelea mradi wa SGR kwa kutumia treni yenye kiwango cha kimataifa kutokea stesheni ya Dodoma hadi stesheni ya Igandu iliyopo jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Gerson Msigwa amewasihi viongozi wa kimila wazidi kuliombea taifa pamoja na mradi wa SGR ili nchi izidi kupata maendeleo na wananchi waendelee kunufaika na matunda ya nchi.

“Nawaomba sana wazee wangu muendelee kusimamia maadili, mila na desturi za watanzania na utulivu wa wananchi ili na miradi hii mikubwa ya kimkakati izidi kulindwa na kutunzwa na sisi wenyewe” alisema Msigwa.

Pia alieleza kuwa mradi wa SGR umegharimu fedha nyingi kwa vipande vitano vya mradi na ni reli ya kwanza inayotumia nishati ya umeme yenye urefu zaidi barani Afrika.

Mkurugenzi Mkuu kutoka TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa alisema kuwa Machifu wana nafasi kubwa ya kuzungumza na jamii ili wazidi kuwa walinzi wa miundombinu ya reli na kwa kufanya hivyo inaweza ikadumu miaka hata mia moja kwa kunufaisha na vizazi vijavyo.

“Treni hii italeta maendeleo makubwa sana katika taifa letu kwa kurahisisha safari za mbali kufika kwa haraka zaidi” alisema Ndugu Kadogosa.

Mwenyekiti wa Machifu nchini Chifu Antonia Shangalai alieleza kuwa viongozi hao wa kimila wamejifunza vitu vingi kwa kujionea mradi huo na kujua asilimia za mradi kwa vipande vyote vya ujenzi na kuahidi kuwa walinzi madhubuti wa miundombinu ya reli.

“Sisi tutasimamia na sehemu zote ambapo reli inapita kama kuna machifu watasimamia vyema jamii zao, reli hii ni yetu na inafaida kwetu sote” alieleza Chifu Shangalai.

Shirika la reli linatarajia kuanza safari za treni ya abiria kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma mnamo tarehe 25 Julai, 2025.