Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​MABEHEWA MAPYA YA METER GAUGE YAANZA SAFARI RASMI KUELEKEA KIGOMA


news title here
15
December
2022

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania – TRC Masanja Kadogosa ameruhusu treni ya abiria yenye mabehewa mapya 21 ya Meter Gauge - MGR yaliyonunuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Kigoma Disemba 15, 2022.

Mkurugenzi Mkuu ameeleza kuwa mabehewa mapya ya MGR yamenunuliwa na serikali ili kuongeza ufanisi wa shirika na kuboresha huduma ya usafiri wa abiria nchini na kuongeza kuwa Mamlaka

ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini – LATRA imetoa ridhaa ya mabehewa hayo kusafirisha abiria baada ya majaribio ya awali kufanyika.

“Majaribio yanafanyika kwa mujibu wa sheria, tulikwenda Morogoro tumerudi na tumepewa cheti baada ya kuthibitishwa na LATRA kwamba yanakidhi mahitaji kusafirisha abiria, hivyo abehewa haya yanakwenda Kigoma yakirudi yanakwenda Arusha” alisema Kadogosa

Kutokana na adha ya usafiri wanayopata abiria nchini hususani kipindi cha sikukuu na mapumziko mwisho wa mwaka Kadogosa amesema kuwa idadi kubwa ya abiria katika kipindi hicho hivyo imepelekea serikali kuamua kununua mabehewa mapya ili kuongeza idadi ya safari za treni na kuwahudumia wananchi.

“Tunaelekea kwenye msimu wa sikuu na mwaka mpya, ndugu zetu wengi wanarudi nyumbani kusalimia lakini kuanzia Januari wataanza kurudi kwa wingi Dar es Salaam, wasiwe na wasiwasi mwaka huu tutakuwa zaidi ya mwaka jana.

Tumejipanga vizuri sana kuhakikisha hakuna presha ya usafiri wakati huu wa sikukuu hatutaongeza nauli bali tutahakikisha treni hii inakwenda Kigoma ikirud inakwenda Arusha lakini nyingine” alisema Ndugu Kadogosa.

Kaodogosa amesisitiza kuwa “ujio wa mabehewa unapunguza adha ya abiria kugombania tiketi, haya yako 22 na mengine yako 22, kwasababu watu wengi wanapenda kusafiri na Deluxe kwahiyo ni jambo zuri sana”

Baadhi ya wananchi wanaosafiri na treni hiyo kuelekea Kigoma wameonesha kufurahishwa na juhudi za serikali kuongeza mabehewa ya abiria na pia kupendekeza kuwa na uwezekano wakuleta mabehewa mengi zaidi.

“Treni inasaidia sana ukilinganisha na mabasi kwenye suala la nauli, nawaambia wananchi waongezeke kuja kukata tiketi” alisema bwana Modest Ernest

Serikali ya JamhurI ya Muungano waTanzania ikiongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuboresha sekta ya reli ili kutoa huduma bora kwa wananchi wanaotumia usafiri wa reli nchini kwa kununua mabehewa, vichwa na mitambo ya ukarabati wa reli ya zamani – MGR na reli ya kisasa – SGR. Sambamba na hayo Serikali inaendelea na ujenzi wa reli ya kisasa Dar es Salaam – Mwanza na hivi karibuni kipande cha Tabora – Kigoma kinarajiwa kuanza ujenzi.