Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​KIKAO KAZI CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI TRC


news title here
02
April
2023

Shirika la Reli Tanzania - TRC limefanya kikao cha baraza la wafanyakazi TRC jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Bandari tarehe 30 na 31 mwezi Machi 2023.

Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi TRC Vincent Tangoh amesema lengo la kikao cha baraza la wafanyakazi ni kumshauri mwajiri kwa kushirikiana na menejimenti namna ya kuendeleza Shirika, baraza hili limeundwa na wawakilishi wa wafanyakazi kutoka idara na kanda zote.

"Baraza hili limeundwa kwa mujibu wa Sheria na hii inasaidia kwa wafanyakazi kupata ushirikishwaji wa majukumu yote yanayoendelea ndani ya shirika" amesema Tangoh.

Mwenyekiti wa wafanyakazi wa TRC Godfrey Siwingwa amesema baraza litasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi katika idara na Kanda zote kupitia wawakilishi kwa kushirikiana na menejimenti.

"Kwahiyo hili baraza litasaidia sana wafanyakazi kujua na kupata haki zao stahiki kutoka kwa mwajiri, pia menejimenti itapata haki ya kuwaambia wajumbe nini kifanyike kwa wafanyakazi ili kuweza kutimiza malengo ya kuboresha shirika" ameongeza Godfrey Siwingwa.

Wajumbe wa Baraza wametembelea mradi wa SGR kipande cha kwanza ambacho ni Dar es Salaam - Morogoro ili kuona miundombinu ya ujenzi wa SGR.

Mjumbe kutoka Morogoro TRC Bi. Asha Bakari ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kuiamini TRC na kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa reli ya kisasa.

"Wafanyakazi wa TRC tunatakiwa kuwa mabalozi wazuri katika kulinda huu mradi ili kuutunza kwaajili ya maendeleo ya watanzania" amesema Bi. Asha.

Bi. Oliva Benedict, mjumbe kutoka idara ya fedha makao makuu TRC amesema anaishukuru menejimenti kwa kuonesha ushirikiano kwa viongozi wa chama cha wafanyakazi na wajumbe wa idara zote za wafanyakazi katika uundaji wa baraza la wafanyakazi, pia ameipongeza TRC kwa kusimamia ujenzi wa reli ya kisasa kwani inaifanya Tanzania kuwa mfano wa kuigwa barani Afrija kupitia miundombinu ya SGR.