Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​KAMATI YA BUNGE PIC YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUENDELEZA MRADI WA SGR


news title here
28
March
2023

Kamati ya bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati Mhe. Jerry Silaa yafanya ziara katika mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR Mwanza – Isaka, Machi 28, 2023.

Kamati imefanya ziara ikiwa nalengo la kuona maendeleo ya mradi pamoja na kuona thamani ya uwekezaji wa mitaji ya umma ambapo Serikali imewekeza fedha nyingi kutekeleza mradi wa SGR kuanzia Dar es Salaam kuelekea Kigoma na Mwanza.

“Sisi tumekuja kuangaliauwekezaji wa mitaji ya umma, Serikali inawekeza fedha nyingi, vipande hivi sita vina thamani ya takribani Dola za Marekani Bilioni 10 kwahiyo ni uwekezaji mkubwa ambao watanzania wanapaswa kujua lakini vilevile Bunge kusimamia na kuishauri Serikali” alisema Mhe. Silaa

Mhe. Silaa amesema kuwa mradi wa SGR ulianza muda mrefu lakini mpaka kufikia 2021 Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani kulikuwa na vipande viwili ambavyo ni Dar es Salaam – Morogoro na Morogoro - Makutupora, lakini katika kipindi cha miaka miwili ya Dkt. Samia vipande vyote vina wakandarasi na kazi inaendelea.

“Kamati leo imefanya ziara kukagua TRC ambayo inasimamia mradi wa SGR inayojengwa kuanzia Dar es Salaam hadi Mwanza na Disemba 2022 Serikali ilisaini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Tabora hadi Kigoma” alisema Mhe. Silaa

Mwenyekiti kwa niaba ya Kamati amepongeza na kuwatia moyo TRC wanaosimamia mradi na kusema kuwa kipande cha Mwanza - Isaka kimeshakamilishwa kwa asilimia 28 hadi kufikia Februari 2023, kazi inaenda vizuri, pia ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendeleza miradi yote ya kimkakati.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TRC Prof. John Kondoro amesema kuwa “Tumepokea kamati ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya umma na wamekuja kutembelea mradi, kuna mambo ambayo wameona na wameeleza. Maendeleo ya mradi ni mazuri kwasababu mkandarasi yuko ndani ya mpango kazi uliowekwa katika hatua za kukamilisha mradi ambao mpaka sasa yuko asilimia 28, tunaamini kwa kasi anayokwenda nayo atamaliza ndani ya muda uliopangwa”

Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma ambao ni wawakilishi wa wananchi walipata fursa ya kuona kazi iliyofanyika na wameangalia maendeleo ya mradi kwa ujumla, wameona vipande ambavyo tayari vimeshajengwa, wameona sehemu mbalimbali ambazo maandalizi tayari ikiwemo jijini Mwanza kwajili ya ujenzi wa daraja, wametembelea Seke kuona kiwanda cha mataruma ambacho kinazalisha mataruma 1,600 kwa siku.

Menejimenti ya Shirika la Reli Tanzania imepokea maelekezo yaliyotolewa na kamati kuhakikisha Shirika linasimamia mradi uweze kuisha ndani ya muda uliopangwa kwani ni matarajio ya Serikali na Wananchi kwamba mradi utaisha kwa wakati ili waweze kunufaika na kile walichowekeza.