Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAZIRI MBARAWA ATANGAZA RASMI SHERIA MPYA YA RELI TANZANIA


news title here
09
May
2018

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa ametangaza rasmi kuanza kutumika kwa Sheria mpya ya Reli Na. 10 ya mwaka 2017. Katika tukio hilo lililofanyika mbele ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Prof. John Wajanga Kondoro. Waziri amesema wafanyakazi waliokuwa RAHCO na TRL watahamia katika shirika la Reli na kuwa mali na madeni yote ya RAHCO na TRL yatahamishiwa kwenye Shirika la Reli Tanzania(TRC).

Katika hatua nyingine mhe. Waziri alimtangaza Bw. Masanja Kadogosa kuwa ameteuliwa NA Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi mpya wa shirika la reli na Prof Kondoro John atakuwa ndio Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Shirika hilo.

Serikali kupitia Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 13 septemba 2017 lilipitisha kuanzishwa kwa sheria ya Reli ya Tanzania. Aidha, tarehe 8 Oktoba 2017, Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt John Pombe Magufuli aliridhia sheria tajwa, na tarehe 13 Oktoba 2017 sheria ya Reli Tanzania ilitangazwa kwenye gazeti la serikali.

Lengo kuu la Sheria ya Reli Tanzania ni kutoa huduma bora ya usafiri kwa njia ya reli, utunzaji na uendeshaji wa miundombinu ya Reli.

Matokeo ya kutungwa kwa sheria ya Reli ni pamoja na kufuta sheria ya Reli Na.4 ya mwaka 2002 na kufutwa kwa iliyokuwa kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) na kampuni ya Reli Tanzania(TRL).