Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAZIRI MKUU MSTAAFU KENYA RAILA ODINGA AMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA UAMUZI WA UJENZI WA RELI YA KISASA – SGR.


news title here
21
March
2019

Waziri mkuu mstaafu wa Kenya Mhe. Raila Odinga atembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Morogoro Machi 21, 2019.

Mhe. Raila Odinga akiambatana na wenyeji wake mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRC Prof. John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli

Tanzania -TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa pamoja na wahandisi wa Shirika la Reli Tanzania, alipata fursa ya kuona ujenzi wa Daraja linaloanzia stesheni ya Dar es Salaam hadi Ilala, utandikaji wa reli pamoja na usimikaji wa nguzo za umeme ukiendelea eneo la Vingunguti Dar es Salaam.

Mhe. Odinga amefurahishwa na kutoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa uamuzi wa kujenga reli ya kisasa - SGR ambayo ina umuhimu katika kuchochea maendeleo ya uchumi, viwanda na biashara Tanzania na nchi jirani za Afrika Mashariki.

Alisema Odinga “sisi kama wakenya tutatumia reli hii kudumisha uhusiano wetu na Tanzania katika sekta ya uchukuzi, uchumi na viwanda, tunataka kufanya biashara na majirani zetu Rwanda, Burundi mpaka Uganda"

Aidha, Mhe. Odinga amefurahishwa na kuipongeza Tanzania na Shirika kwa kutoa ajira kwa watanzania katika ujenzi wa reli ya kisasa ambapo, asilimia 92 ni watanzania na asilimia 8 ni wafanyakazi wa kigeni.

Hata hivyo alitoa ushauri kwa vijana wa Tanzania kutumia mradi huu mkubwa wa SGR kupata ujuzi katika kada mbalimbali hata pale mkandarasi atakapoondoka nchini ujuzi utabaki kwa watanzania.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania –TRC Prof. John Kondoro pamoja na Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu

Kadogosa, wamemshukuru Mhe. Raila Odinga kwa kutembelea Mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro chenye urefu wa kilometa 300, ambao umefikia asilimia 45.8 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2019.

Mkurugenzi Mkuu ameongeza kuwa, ugeni huo mkubwa ni heshima kwa taifa na unadumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Kenya kibiashara na kiuchumi.