Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

FAFANUA KUHUSU KUCHELEWA KUANZA UTOAJI HUDUMA KWA KUTUMIA TRENI YA UMEME (SGR) -MSEMAJI MKUU WA SERIKALI


news title here
01
June
2023

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo ambae pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Bwana Gerson Msigwa ametoa ufafanuzi kuchelewa kuanza utoaji wa hudua za usafiri wa reli kwa kutumia treni ya umeme zitakazo tembea katika reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) mwezi Mei 2023 kama ilivyo tarajiwa.

Akiongea na waandishi wa Habari Jijini Dodoma Mei 31, 2023 Bwana Msigwa ameeleza kuwa kuchelewa kuanza kwa huduma kwa kutumia treni ya umeme kulitokana na kutokamilika kwa matengenezo ya vichwa viwili vya kuvutia treni kwa wakati kutokana na sababu za kimsingi na kupelekea majaribio ambayo yalitarajiwa kuanza Mei, 2023 kusogezwa mbele mpaka Julai, 2023.

"Hatuwezi kuendesha treni bila vichwa ,baada ya kuvunjika mkataba kati ya TRC na kampuni ya Eurowagon ya Nchini Uturuki mkataba wa matengenezo ulihamishiwa kampuni ya Lueckermeier Transport and Logistic GMBH ya Nchini Ujerumani,kumekuwa na changamoto ya utengenezaji wa vichwa kutokana na shida ya upatikanaji wa vipuri vinavotumika katika ukamilishaji wa vichwa vya treni kutokana na ugonjwa wa Uviko 19 na mambo ya vita vya Russia na Ukraine vimesababisha kuharibika kwa uchumi duniani hizo ni sababu za msingi zilizopelekea ucheleweshaji huo" Amesema Msigwa.

Bwana Msigwa ameendelea kusema kwamba kichwa cha kwanza cha treni Kati ya vichwa viwili vinayvo tengenezwa nchini ujerumani na kampuni ya Lueckermeier Transport and Logistic GMBH kitawasili mwezi Julai mwaka huu na kuwezesha shughuli za majaribio ya treni hizo kuanza.

Aidha, Msemaji Mkuu ameongeza kuwa baada ya kupokea Mabehewa 14 Kati ya 59 kutoka kampuni ya Hyundai Rotem ya Nchini Korea Oktoba, 2022 na Mabehewa sita (6) kati ya thelathini(30) yatakayo wasili hivi karibuni ambayo yamekarabatiwa nakutengenezwa na kampuni ya Lueckermeier Transport and Logistic GMBH ya Nchini ujerumani na kufikia kwenye ubora wa kiwango cha zaidi ya asilimia 85 yatawezesha kuanza kwa shughuli za uendeshaji haraka kama ilivotarajiwa.

"Watanzania msiwe na wasiwasi majaribio ya treni yataanza kama tulivosema Mwezi wa Saba mwaka huu baada ya kichwa cha treni kufika na baadae kuanza kutoa huduma rasmi " Alisema Msigwa.

Bwana Msigwa aliongeza kusema Serikali inatekeleza mradi wa SGR kwa awamu mbili , awamu ya kwanza ya utekelezaji huo ni ujenzi wa Reli ya SGR kutoka Dar Es Salaam hadi Mwanza na kwa awamu ya pili ya utekelezaji ni kutoka Tabora hadi Kigoma .