Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

BILIONI 379 ZA WEKEZWA KUBORESHA RELI YA MGR - KALIUA-MPANDA


news title here
25
October
2026

Wizara ya Uchukuzi imesema serikali imewekeza shilingi Bilioni 379 kuboresha reli ya MGR kipande Cha Kaliua- Mpanda (km 210).

Hayo yamesemwa Oktoba 10, 2026 na Waziri wa Uchukuzi Mhe.Prof Makame Mbarawa Mnyaa katika siku ya pili ya ziara ya Kikazi ya kukaagua ujenzi na maendeleo ya miradi ya reli ya SGR kipande cha 2,3,4,5 &6.

Akiwa katika kiwanda cha uzalishaji wa mataruma ya zege mahususi kwaajili ya mradi wa maboresho ya reli ya MGR, Kaliua-Mpanda, kilichoko Kijiji cha Uyumbu, Wilayani Kaliua Mkoani Tabora, Prof. Mbarawa, amesema Katika kuwezesha maboresho hayo TRC inaendelea na uzalishaji mataluma ya zege lengo likiwa ni kuondoa mataluma ya chuma yaliokuwa yakitumika awali ili kuiongezea reli ya MGR uwezo wa usafirashaji hasa wa mizigo.

Kwa namna nyingine uzalishaji wa matalamu ya zege nchini umeisadia serikali kupunguza gharama za uzalishaji zliizokuwa zikitumika katika uzalishaji wa mataluma ya chuma ambapo taluma moja la chuma lilikuwa likitengenezwa Kwa shilingi 360,000/ ukilinganisha na uzalishaji wa mataluma ya zege ambapo taluma moja la zege uzalishwa kwa shilingi 160,000/-

Hii maanake yake ni kwamba fedha zilizopungua kutokana na uzalishaji wa mataluma ya zege zitatumika katika Uwekezaji na uboreshaji maeneo mengine ya miradi ya reli.

Licha ya kwamba viwanda vya uzalishaji mataluma nchini vimetoa Ajira nyingi Kwa vijana Waziri Mbarawa amesema kuwa imewapa fursa vijana wengi kujifunza taaluma ya uzalishaji mataluma na kuifanya Tanzania kuwa kitivo cha mafunzo Kwa nchi zingine za Kiafrika .

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Mha.Machibya Shiwa amesema kuwa pamoja na uboreshaji wa reli ya MGR unaoendelea kufanyika TRC imejikita katika uzalishaji wa mataluma ya zege kwanza kuongeza ufanisi wa reli ya MGR kubeba mizigo na pili kuongeza uzito wa reli ili kusafirisha mizigo Kwa haraka na Kwa Muda mfupi.

Mhandisi Machibya amefafanua kwamba taluma moja la zege linauzito wa kilo 250 ukilinganisha na uzito wa taluma la chuma ambalo uzito wake ni kilo 39.7 hii

inamaanisha kwamba mataluma ya zege yanauwezo mkubwa wa kuimili uzito mkubwa wa mizigo na kuongeza spidi ya treni.

Aidha, Mhandisi Machibya ameeleza kuwa uzalishaji wa mataluma ya zege hapa nchini ndani ya kipindi miaka 2 kutoka sasa reli yote ya MGR itakuwa imebadilishwa kutoka mataluma ya chuma kwenda mataluma ya zege hivyo kuifanya reli ya MGR kusafirisha mizigo mikubwa Kwa wakati mmoja na haraka zaidi kuliko sasa .

Mkakati wa Serikali chini ya Uongozi wa Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa kitovu Cha kuunganisha nchi jirani kupitia biashara na muunganiko chanya ,pia kuwaleta watanzania pamoja kupitia shughuli za Kila siku za kiuchumi na kijamii.u