Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAZIRI MBARAWA AAGIZA TRC, TPA NA TASAC KUKAA PAMOJA KUHUSU MIZIGO YA NJE KUPOKELEA BAHI/ISAKA*


news title here
24
October
2026

Wizara ya Uchukuzi imeziagiza Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) pamoja na Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), kukaa pamoja na kuvifanya vituo vya Bahi na Isaka, kuwa stesheni za kupokea mizigo moja kwa moja kutoka nje ya nchi.

Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, ametoa maagizo hayo katika stesheni ya mizigo ya Bahi, Dodoma, katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku nne, kukagua maendeleo ya Ujenzi wa mradi wa SGR kipande cha pili mpaka cha tano.

Aidha kufuatia ziara yake ya hivi karibubi nchini Misri, amezitaka pande tatu hizo kutuma wataalamu kwenda nchini humo kujifunza

namna walivyofanikiwa kuufanya mfumo wa usafirishaji mizigo kuhusisha ushirikiano kati ya reli, bandari na kampuni za usafirishaji akitolea mfano wa kampuni za kimataifa za usafirishaji wa mizigo, kama CMA, CGM na Emirates ambazo pia zina shughuli nchini Tanzania.

Mojawapo ya mambo ambayo Prof. Mbarawa ameyagusia ni mafunzo juu ya kuchaji gharama za mizigo na uandaaji wa bill of Lading (B/L) yaani hati ya Upokeaji na Usafirishaji wa Mizigo kwa njia ya Bahari.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Uchukuzi, amelipongeza Shirika la reli Tanzania (TRC), kwakuwa wabunifu ambalo sasa reli za SGR na MGR zinashirikiana kusafirisha mzigo kutoka SGR (Bahi) na kuhamishiwa kwenye MGR (hapohapo Bahi) kisha kupelekwa Isaka.

Prif. Mbarawa, amesema ubunifu huo ni mzuri kwakuwa unaenda kuchangia kupunguza msongamano wa makontenag katika Bandari ya Dsm.

Amesema lengo kuu ni kutoa kontena 1000 kwa siku na kuifanya Bandari ya Dsm ambayo kila siku inatoa kontena 3,000 (20ft) kupumua.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Mhandisi Machibya Shiwa, amesema kukamilika kwa Kituo cha Uhamishaji Mizigo cha Bahi (Bahi Transshipment) kumeongeza ufanisi wa usafirishaji wa makontena.

Mha.Machibya amesema kuwa safari ya mizigo kutoka Dar es Salaam hadi Bahi inachukua takribani saa tano hatua inayochangia kurahisisha upatikanaji wa mizigo kwa wateja ndani ya saa 24 hadi Isaka.

Aidha, Mhandisi Shiwa amesema miongoni mwa mafanikio ya TRC ni kusafirisha abiria milioni 7.6 tangu kuanza kwa huduma za uendeshaji wa SGR mwezi Julai 2024.

Maendeleo ya reli ya SGR ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha usafiri na usafirishaji nchini, kupunguza msongamano bandarini, kuongeza ufanisi wa biashara na kuimarisha huduma kwa wananchi na wafanyabiashara.