Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WASANII, WANAMICHEZO, WASHEREHESHAJI WAFURAHISHWA NA MRADI WA SGR


news title here
18
February
2019

Wasanii, Wanamichezo, Wanahabari na Washereheshaji wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda watembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro kwa lengo la kuona maendeleo ya Mradi pamoja na kujifunza kuhusu mradi wa SGR mapema mwezi Februari 2019.

Wasanii, Wanamichezo, Wanahabari na Washereheshaji katika ziara walipata fursa ya kujifunza na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa pamoja na Meneja Mradi wa SGR Dar- Moro Mhandisi Machibya Masanja katika Stesheni ya Kamata eneo ambalo linajengwa daraja lenye urefu wa Kilometa 2.5n kutoka Stesheni ya Dar es Salaa hadi Ilala kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Morogoro kwa kutumia treni ya kisasa ya Deluxe.

Aidha Wasanii, Wanamichezo, Wanahabari na Washereheshaji wamefurahishwa na Mradi wa SGR kwa kuwa una maslahi makubwa kwa wasanii na watanzania kwa ujumla na wameahidi kuwa Mabalozi kueleza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano ukiwemo Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR ambao unatekelezwa na Serikali kwa pesa za watanzania walipa kodi.