Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

MAAFISA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO KUTOKA ZANZIBAR WATEMBELEA TRC.


news title here
22
June
2023

Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar watembelea Shirika la Reli Tanzania kujifunza na kubadilishana uzoefu wa majukum ya kazi za habari, Juni 22, 2023.

Maafisa wapatao 25 wakiongozwa na Mkurugenzi wa Habari Malezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bwana Hassan Khatib Hassan wametembelea TRC kwa lengo la kujifunza mbinu , njia na ubunifu wa mawasiliano unaotumiwa na kitengo cha Habari na Mawasiliano ya Umma, Shirika la Reli Tanzania katika kuhabari umma na kujenga uhusiano mzuri baina ya Shirika la Reli Tanzania na umma.Haya yote yanafanyika kuendelea kuimarisha na kuboresha ufanisi katika vitengo vya Habari Tanzania.

Akiongea wakati wa ziara ya kikazi Bwana Khatib Hassan amesema kuwa ziara hiyo ya kikazi imelenga kutembelea taasisi zinazofanya vizuri katika mawasiliano ya umma Tanzania Bara na TRC ni miungoni mwa taasisi inayofanya vizuri.Wanahabari kutoka Zanzibar wamekuja kubadilishana uzoefu wa kazi, kujifunza mbinu mbalimbali za kuhabarisha umma kwa kutumia muongozo wa mkakati wa mawasiliano kwa umma ambao ni vema kila kitengo cha habari kuwa na muongozo huu kutokana na asili ya majukum ya taasisi husika.

“Lengo la ziara yetu kuja Tanzania Bara ambayo tumeanzia Dodoma na tunamalizia hapa Dar Es Salaam ni kujifunza kwa wenzetu wa tasnia hii ya habari na wasiliano na kupata uzoefu , tunashukuru Mungu ametuwezesha kuja leo hii , kwa kweli hapa TRC tumejifunza mengi ambayo hatukuyajua hapo awali,nathubutu kusema kuwa tumepata zaidi ya yale tulio yatarajia,wenzetu wa TRC wametupa mengi ambayo kwetu sisi ni mageni” Alisema Bwana Khatib.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Ndugu Masanja Kungu Kadogosa amesisitiza kuwa Maafisa Habari na Uhusiano wa Taasisi mbalimbali za serikali wanapaswa kupewa ushirikiano na viongozi wa taasisi au mashirika ili waweza kutoa taarifa na kuhabarisha umma kwa usahihi na haraka kuhusiana na masuala , kazi, juhudi na utekelezaji wa miradi unazofanywa na serikali kupitia taasisi , mashirika na mamlaka mbalimbali.

“Masuala ya kuhabarisha umma sio siasa kama wengi wanavyodhani, watu wanapoona vitu vinafanyika kama matakwa yao na viongozi wanazungumza masuala mbalimbali ni muhimu katika nchi, kitu ninachoweza kusema ni kwamba mambo ya mahusiano na mawasiliano kwa umma yanatakiwa yaanzie juu kwenye uongozi wa taasisi” Alisema Kadogosa.

Kadogoa aliongeza kuwa” Miongoni mwa taasisi za serikali, TRC inafanya vizuri sana katika masuala ya kuhabarisha umma kupitia mbinu mbalmbali na vyombo mbalimbali vya habari, inawezekana isiwe asilimia mia moja lakini tupo vizuri na mimi kama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika napenda ili lifanyike, miaka mitano iliopita TRC kwenye mawasiliano ya umma haikuwa hivi”.

Maafisa Habari , Mawasiliano na Uhusiano kwa umma ni tasnia muhimu sana katika taasisi za serikali kwa lengo la kuhabari umma wa kitanzania ili kuendelea kujenga mahusiano mazuri na uelewa baina ya serikali na wananchi .