Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

ZOEZI LA ULIPAJI FIDIA KUPISHA UJENZI WA RELI YA KISASA SGR MORGORO – MAKUTUPORA LAZIDI KUPAMBA MOTO JIJINI DODOMA


news title here
14
September
2020

Shirika la Reli Tanzania TRC linaendelea na zoezi la ulipaji wa fidia jijini Dodoma kwa wananchi ambao maeneo yao yametwaliwa na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR kipande cha Morogoro Makutupora,hivi karibuni septemba 2020.

Zoezi hili ni muendelezo wa awamu kadhaa za ulipaji wa fidia jijini humo, ambapo maafisa kutoka shirika la reli Tanzania wapo jijini humo kuhakikisha wananchi ambao maeneo yao yalitwaliwa na mradi,wanapata stahiki zao kama inavyotakiwa. Pamoja na maeneo mengine ya jijini DodomaWananchi ambao wanalipwa fidia katika awamu hii ya zoezi la ulipaji fidia ni pamoja na wale wa maeneo ya Ihumwa,Pinda,Mkalama “A”,Miganga,Muungano “B” na Bwawani.
Mthamini kutoka shirika la Reli Tanzania, Bi. Benlulu Lyimo, amesema kuwa katika zoezi hili la siku 10 linalotarajiwa kumalizika tarehe 20 mwezi Septemba 2020, wafidiwa kutoka mitaa 22 ya jiji la Dodoma na vijiji 9 vya wilayani Bahi wanatarajiwa kulipwa.
“Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania TRC,imejipanga kulipa wafidiwa wote na tunawahakikishia kuwa kila ambae eneo lake limetwaliwa na mradi ni lazima atalipwa stahiki zake” aliongeza Bi. Lyimo.
Zoezi hili la ulipaji fidia linaenda sambamba na kuwashauri wafidiwa juu ya namna bora ya matumizi ya fedha hizo ili kuwaletea wananchi hao maendeleo.
Aidha simamizi wa masuala ya kijamii,Bi.Catherine Mwakigali amesema kuwa “kuna wengine wanafikiria kufanyia starehe,kwahiyo tunawashauri kuzitumia vizuri pesa hizo ikiwemo kwenda kuanzisha makazi mapya au shughuli nyingine za kimaendeleo kama vile biashara”
Kwa upande wake mmoja wa wananchi waliolipwa fidia zao,Bw.Hamisi Samson amesema “kwa kutumia fedha hizi nitajenga nyumba nyingine,nitasomesha watoto na shughuli nyingine za kimaendeleo”
Zoezi hili ni utekelezaji wa ahadi ya kuwa kila mwananchi ambae eneo lake limetwaliwa na mradi, atalipwa na mpaka sasa ujenzi wa reli ya kisasa SGR katika kipande cha Morogoro - Makutupora,umefikia zaidi ya 35%