WAZIRI WA VIWANDA NA UWEKEZAJI SUDAN KUSINI ATEMBELEA MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA - SGR.
June
2019
Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Sudan Kusini Ndugu Paul Mayomu atembelea Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa-SGR kipande cha Daresalaam - Morogoro, Ziara hiyo imefanyika hivi karibuniJune , 2019.
Aidha, katika ziara hiyo iliongozwa na mwenyeji wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe, walipata fursa ya kuona maendeleo na hatua tofauti za ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR ukiwemo ujenzi wa stesheni kuu ya Daresalaam, madaraja, na utandikaji wa reli unao endelea maeneo ya vingunguti jijini Dar Es Salaam.
Waziri Mayomu ameipongeza Tanzania kwa kuamua kujenga Reli ya Kisasa - SGR ambayo ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya uchumi, viwanda na biashara katika Taifa na nchi jirani.
Hata hivyo, Waziri Mayomu ameeleza kuwa reli hii itakapo kamilika itakuwa chachu ya maendeleo kwa nchi zote mbili pia itadumisha uhusiano katika sekta ya uchukuzi, viwanda na biashara kati ya Tanzania na Sudan ya Kusini.
Kwa upande wake, Waziri Kamwelwe amempongeza waziri Mayomu kwa kuja Tanzania ambayo ni heshima kwa Taifa na kujionea maendeleo yanayofanyika katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi katika ujenzi wa reli ya kisasa ambayo ni chachu ya maendeleo baina ya nchi hizo mbili.
Waziri Kamwelwe ameahidi kudumisha uhusiano kupitia reli ya kisasa hasa katika sekta ya viwanda, biashara na uchumi.