Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AFANYA UFUNGUZI WA RELI YA TANGA - MOSHI/ KILIMANJARO


news title here
21
July
2019

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe . Kassim Majaliwa amefanya ufunguzi wa njia ya reli ya Tanga mpaka Moshi / Kilimanjaro katika hafla iliyofanyika mjini Moshi , Kilimanjaro hivi karibuni Julai 2019, iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wa vyama pamoja na wa dini.


Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amelipongeza Shirika la Reli Tanzania -TRC kwa Kurejesha njia ya Tanga-Moshi ambayo takribani zaidi ya miaka 12 ilikuwa haifanyi kazi. Waziri Mkuu amesema kuwa mafanikio haya ni utekelezaji wa sera ya kitaifa na Mkakati wa Nchi kuinua sekta mbalimbali za kimkakati ili inchi ya Tanzania ifikie Uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Waziri mkuu aliongeza kuwa juhudi na kujitoa kulikofanyika kurejesha njia ya reli kuanzia Dar es Salaam hadi Tanga na kisha kuelekea Moshi ,Kilimanjaro ni uamuzi wa busara uliokuja kwa wakati na unaoshamirisha azima yetu ya kuchochea ukuaji wa uchumi lakini na kuyabadili maisha ya wananchi kupitia huduma bora za usafiri na uchukuzi .
“ Kamwe hatuwezi kufikia hadhi hiyo muhimu kiuchumi bila kuwa na miundombinu imara ikiwemo ya reli “ amesema Mhe. Kassim Majaliwa.


Aidha Waziri Mkuu amebainisha kuwa Tanzania inapakana na nchi zaidi ya tano ambazo zinategemea sana miundombinu ya nchi ya Tanzania ya usafirishaji na uchukuzi ndani ya nchi ili kupitisha bidhaa. Pia aligusia juu ya mradi mkubwa wa kihistoria wa SGR unaoendelea kuanzia Dar es Salaam hadi Mokutopola na kusema kuwa Serikali ya awamu ya tano imewekeza takribani Shilingi Bilioni 7.2 fedha za walipa kodi kutekeleza mradi huo .

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Atashasta Nditiye ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kutoa fedha pia amepongeza bodi na uongozi wa Shirika la Reli Tanzania katika ufuatiliaji na utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya ufufuaji wa Shirika na njia mbalimbali za reli zilizokufa kwa miaka mingi hapa nchini. Hata hivyo Naibu Waziri ametoa rai kwa wafanyazi wa Shirika la Reli na watanzania kwa ujumla kuwa walizi wa miundombinu ya reli ambayo ni kichocheo kikubwa cha uchumi wa nchi yetu.


“TRC limepewa dhamana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia uhuishaji na utendaji wa shirika pamoja na kuboresha huduma za reli “ amesema Mhe . Nditiye .