Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

​WAZIRI MKUU AFURAHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA RELI YA KISASA - SGR


news title here
07
August
2020

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa afurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa reli ya kisasa – SGR kipande cha Dar es Salaam – Ruvu Agosti 7, 2020.

Katika Ziara hiyo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa aliambatana na Naibu Waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Mhe. Atashasta Nditiye,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Alhaji Kunenge,Mkuu wa Mkoa wa pwani Mhe. Mhandisi Ndikilo,Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi TRC Prof John Kondoro, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania – TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa, Wakuu wa Vyombo vya Usalama, Wahandisi kutoka Yapi Merkezi na Viongozi wengine wa Serikali.

Ziara hiyo ambayo imefanyika na Waziri Mkuu kwa lengo la kuona maendeleo ya Mradi wa reli ya kisasa ambayo mpaka sasa ujenzi wake umefika zaidi ya asilimia 80 ,pia Mradi wa SGR ni kati ya mradi mkubwa wa Serikali unayosimamiwa na kuratibiwa na TRC chini wa serikali ya awamu ya Tano iliyo chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli.

Ziara ilianza katika stesheni ya Dar es salaam ambapo Waziri alipata kuona stesheni ya Dar es salaam yenye umbo la madini ya ‘Tanzanite ‘ambayo mpaka sasa ujenzi wake umefika zaidi ya asilimia 80 ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa alimuelezea Waziri Mkuu Maendeleo ya Mradi kwa ujumla ikiwemo Ujenzi wa Stesheni ya Soga, Ruvu,Ngerengere na Morogoro .

Halikadhalika akiongea kwenye Ziara hiyo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amesema nipo kwenye ziara ya kawaida ya kiutendaji ya kufatilia miradi inayojengwa na serikali yetu, miradi inayoandaliwa kwa matumizi ya watanzania wote, leo nimerudi tena mara ya tatu kufatilia miradi huu wa reli ya kisasa na nitapanda treni ya kisasa kutoka Ruvu mpaka Pugu nimeanzia stesheni kubwa ya reli ya Dar es salaam inayofanana na madini yetu na hatua iliyofika mapaka sasa ukiona inavutia, na ujenzi wa daraja lile la kilomita 2.5 unaedelea vizuri sana, na wale wapanda treni wetu watakuwa wanapandia juu haya mambo tulikuwa tunayaona ulaya sasahivi tunayaona Tanzania.

‘’Nimekuja kufanya ukaguzi wa njia hii kutoka Dar es salaam mpaka Ruvu awali nilikuwa naishia Soga na nilipanda treni hiyo kwa umbali kidogo kama kilomita 15, lakini leo hii naambiwa nitapanda kwa umbali mrefu na nimeona kazi kubwa ikifanyika na sehemu kubwa imekamilika kazi inayofanyika ni kuweka nguo za umeme zitakazofanya treni yetu itembee nabtreni itakayotumika ni ya umeme ,wakati wengine wanatumia diesel sisi tumeshahama huko sisi tutatumia umeme na tunao wa kutosha na unaendelea kuzalishwa mto rufiji Tanzania tunakwenda kwenye maendeleo yanayokimbia mno, nawapongea wakandarasi Yapi Merkezi chini ya Usimamizi wa TRC “alisema Waziri Mkuu.

Aliongezea kusema kuwa Serikali imejipanga vizuri kuendele kujenga Reli hii ya kisasa ambao unagharimu fedha zaidi ya tilioni 7 ambazo fedha hizo ni za watanzania ,watanzania tunaweza tukiamua ila wale wachache wasiopenda maendele wataturudisha nyuma sisi wenyewe tulinde miundo mbinu ya Reli, reli hii itajenga uchumi wetu kwa kiasi kikubwa, mradi huu unafaida nyingi kila mahali unapopita basi wananchi wa sehemu hiyo wananufaika.

Naye kwa upande wake Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye amesema kuwa anamshukuru Waziri Mkuu kwa jinsi ambavyo sasa Shirika la Reli Tanzania – TRC unalipa kipaombele cha pekee ndani ya miezi mitatu umetembelea mara mbili hichi ni kitu cha kipekee kabisa.

‘’ Ningependa kukuhakikishia kuwa wakati tumeshafikia asilimia zaidi ya 87 Morogoro na asilimia zaidi ya 36 kufika Dodoma tumeshaanza taratibu za manunuzi za mabehewa ya abiria na vichwa vya kisasa kabisa kwa ajili ya kutoa huduma katika maeneo hayo yaliyobakia, sambamba na huu mradi mkubwa tunaendelea pia kuimarisha reli yetu ya zamani kutoka Da…