Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WAZIRI KAMWELWE AZINDUA KICHWA CHA TRENI, VINGINE SITA KUKAMILIKA HIVI KARIBUNI


news title here
11
October
2020

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua kichwa kimoja cha treni kati ya vichwa saba vilivyofanyiwa ukarabati katika Karakana ya Morogoro, hafla hiyo imefanyika katika Stesheni ya Dodoma Oktoba 11, 2020.

Waziri Kamwelwe amezindua kichwa hiko miongoni mwa vichwa saba ambavyo vimefufuliwa na kurejea katika hali ya utendaji katika Karakana ya reli mkoani Morogoro ambapo vichwa vingine sita viko katika hatua za mwisho za upakaji rangi ili kukamilisha ukarabati wake.

Vichwa hivyo saba vitakapokamilika vitasaidia kazi ya upangaji Behewa za mizigo katika vituo vya Mizigo vilivyopo katika bandari ambazo zinahudumiwa na reli za TRC na kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za usafiri wa abiria na usafirishaji wa mizigo.

Vichwa hivyo saba vitakapokamilika vitasaidia kazi ya upangaji Behewa za mizigo katika vituo vya Mizigo vilivyopo katika bandari ambazo zinahudumiwa na reli za TRC na maeneo mengine, hatimaye kuongeza ufanisi katika utoaji huduma za usafiri wa abiria na usafirishaji mizigo.

Aidha, Waziri Kamwelwe ameeleza kuwa Mradi wa ufufuaji wa vichwa vya treni ni muendelezo wa jitihada za serikali katika kuliwezesha Shirika la Reli kuhudumia wananchi ipasavyo

“Jitihada hizi zinalenga katika kuliwezesha Shirika la Reli kuwa na vichwa vya kutosha kusogeza mizigo na vitatumika hasa katika Bandari ya Kwala na vingine vitapelekwa katika maeneo ya Arusha, Moshi na Dar es Salaam, kukamilika kwa vichwa hivi vitalisaidia Shirika kupambana na changamoto ya kutokuwa na vichwa vya kutosha” aliongeza Mhe. Waziri

Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Lameck Magandi amesema kuwa ukarabati wa vichwa vingine sita upo katika hatua za mwisho na unatarajiwa kukamilika hivi karibuni mwezi Otkoba 2020.

“Mradi wa ukarabati wa vichwa sogeza unaendelea katika karakana ya Morogoro, kimoja tayari kimemalizika na vichwa sita vilivyobaki viko katika hatua za mwisho za kupaka rangi na mwezi huu vitakamilika”

Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania inaendelea na jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya uhakika katika usafiri wa reli nchini, hivyo ili kufanikisha hilo Miradi kadhaa ukiwemo wa Uboreshaji wa Reli ya Kati, Ujenzi wa Reli ya Kisasa, Ufufuaji wa Vichwa vya treni na Ufufuaji wa njia za zamani imekuwa ikitekelezwa kwa wakati mmoja ili kuongeza ufanisi wa Shirika kuhudumia idadi kubwa ya wananchi wanaohitaji kusafiri na kusafirisha bidhaa kupitia mtandao wa reli uliopo kote nchini.