WAZIRI JAFO AONGOZA ZIARA YA VIONGOZI KUONA MRADI WA SGR.

May
2019
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo aongoza wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, Majiji na makatibu tawala wa wilaya katika ziara kuona maendeleo ya mradi wa aujenzi wa reli ya kisasa – SGR katika kambi ya SGR ya Soga Kibaha mkoani Pwani hivi karibuni Mei 2019 Viongozi kutoka mikoa na wilaya tofauti nchini wakiongozwa na mwenyeji wao Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania - TRC Ndugu Masanja Kungu Kadogosa walipata fursa ya kujua maendeleo ya mradi kupitia taarifa ya Mkurugenzi Mkuu TRC aliyoiwasilisha katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwl. J.k. Nyerere kabla ya kuanza ziara kuelekea Soga Kibaha mkoani Pwani ilipo kambi kubwa ya SGR. Lengo la ziara ni kuwajulisha viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya Wilaya na Mikoa kuhusu maendeleo ya Mradi ili waweze kuwa mabalozi katika maeneo wanayoongoza na kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya umuhimu wa mradi wa mkubwa wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa unaoendelea kuanzia Dar es Salaam hadi Makutupora Singida. Waziri Jaffo amempongeza Mkurugenzi Mkuu wa TRC Ndugu Masanja Kadogosa, Uongozi na wafanyakazi Shirika la Reli Tanzania kwa usimamizi mzuri wa Mradi wa SGR na kuwasisitiza waendelee kuchapa kazi ili kuleta tija katika sekta ya uchukuzi nchini. Amesema Waziri Jaffo “Mnafanya vizuri sana katika usimamizi, endeleeni kusimamia jambo hili, Mheshimiwa Rais ametutegemea sana na ninyi anawatumaini sana mnafanya vizuri endeleeni kusonga mbele” Aidha viongozi wamefurahishwa na kazi zinazoendelea katika mradi ikiwemo uzalishaji wa Mataruma katika kiwanda kilichopo Soga pamoja na hatua kubwa zilizofikiwa ambapo hivi sasa Mkandarasi anaendelea na kazi ya kuweka tabaka la pili la kokoto za juu (second layer balast), kuunga reli kwa kutumia umeme na kushindilia kokoto ili kuimarisha tuta (tamping), ujezni wa vituo vya umeme pamoja na usimikaji wa nguzo za umeme, mpaka sasa mradi umefika zaidi ya 50% huku ujenzi ukizidi kuendelea kushika kasi.