Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WANANCHI WA MITAA YA AZIMIO, KIHONDA KASKAZINI NA YESPA WASHUKURU SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWA KULIPA FIDIA ZAO.


news title here
19
August
2020

Wananchi wa Mitaa ya Azimio, Kihonda kaskazini na Yespa vya kata ya Kihonda Mkoni Morogoro Waanza kulipwa fidia zao Agosti 19,2020.

Zoezi hili ambalo ni endelevu linalofanywa na Shirika la Reli Tanzania - TRC chini cha serikali ya Awamu ya Tano limeendelea kulipa Fidia kwa Wananchi waliopitiwa na Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR.

Zoezi hilo limefanywa na maafisa toka TRC na Viongozi wa serikali za Mitaa kama Watendaji wa Mitaa husika na maafisa Ardhi wa Manispaa ya Morogoro Mjini.

Akiongea Katika Zoezi hilo la Ulipaji Fidia Mtendaji wa Mtaa wa Azimio Bwana Geofrey Selekwa amewaomba wananchi wa Mitaa hiyo husika kutoa ushirikiano kwa Maafisa wanaoendesha Zoezi hilo na kusikiliza Maelekezo wanayopewa ili zoezi liende kama lilivyopangwa na kukamilisha kwa wakati uliopangwa ili kuendelea na mitaa mingine inayotarajiwa kulipa hivi karibuni.

Afisa Ardhi wa Manispaa ya Morogoro Steven Awary amewasihi wananchi wa Mitaa hiyo kutumia hiyo fedha watakayopata kuwekeza kwenye ardhi maana ardhi aiozi na kuwasihi wafike kwenye ofisi za Manispaa hizo kuweza kupata viwanja vingine.

Naye Afisa Ardhi wa TRC Bwana Valentino Baraza amewaomba Wananchi wa Mitaa hiyo kupokea Hundi zao na kama kuna malalamiko yoyote waandike barua kwa TRC na kuahidi kutatua changamoto zozote zitakazojitokeza.

Wananchi wa Mitaa hiyo

wamefurahishwa na malipo hayo ya Fidia kwani hawakutegemea kulipwa hivi karibuni kutokana na Mlipuko wa Ugonjwa wa Corona hivyo wanalishukuru Shirika la Reli Tanzania- TRC na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Dr John Pombe Magufuli.