Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WANANCHI NA WAZEE WA MAGINDU WILAYA YA KIBAHA MKOANI PWANI WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KULIPA FIDIA ZAO


news title here
07
September
2020

Wananchi wa Magindu Wilaya ya Kibaha mkoani pwani wamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwa kulipa Fidia zao hivi karibuni Septemba 2020.

Zoezi hilo la Ulipaji Fidia imesimamiwa na kuendeshwa na Maafisa toka TRC wakishirikiana na Viongozi wa Kijiji na kata za Magindu ambapo lilifanyika kwa siku Mbili mfululizo ili kuhakikisha kila mwananchi anayestaili kulipwa Fidia yake analipwa siku hiyo ili kumpisha mkandarasi ambaye ni Yapi Markezi kuendelea na Ujenzi.

Wananchi wa Magindu wamefurahishwa na jinsi zoezi zima lilivyoendeshwa kuanzia siku ya kwanza mpaka ya mwisho “TRC imetujali sana kwa kuja kutulipa Fidia tetesi nyingi tulisikia za kwenda kufata hundi zetu za fidia makao makuu ya Shirika ambapo sisi wengine ni wazee hatuwezi kutembea na kusafiri umbali mrefu lakini nimefurahi wamekuja kwenye serikali hii inatujali sisi wazee “alisema Mzee Konde moja kati ya walipwaji Fidia waliopitiwa na Mradi wa ujenzi wa reli ya Kisasa - SGR .

Mzee Hamisi Jumanne moja kati ya walipwa Fidia ambaye kwa sasa haoni tena kutokana na maradhi ya macho amesema “Maafisa toka TRC wamenifata nyumbani kwangu kunipatia hundi yangu mimi nina umwa huu ni mwaka wa nne Sasa sioni tena lakini nashukuru nimepata hundi yangu kwani kutokana na maradhi haya nikajua sitopatiwa hundi yangu kwani siwezi kutoka nje na kutembea kama mwanzo nashukuru sana TRC na Mkurugenzi wake “.

Afisa Ardhi bwana Valentine Baraza amesema yeyote ambaye amefanyiwa udhamini na bado hajapatiwa hundi yake asiwe na wasiwasi TRC inalipa watu wote waliochukuliwa maeneo yao ili kupisha ujenzi hivyo waandike barua kupitia serikali zao za Mitaa na sisi kitengo chetu cha Ardhi tutakuja upya kufanya uthamini upya hivyo wasiwe na wasiwasi.

Naye kwa Upande wake Mtendaji wa Kata ya Magindu amewashukuru TRC na Serikali kwa Ujumla mana bila serikali kuiwezesha TRC wasingeweza kuja kulipa Fidia ukizingatia serikali imeanza kampeni hivyo sisi watendaji wa Magufuli tunashukuru Mno Jitihada zinazofanywa na serikali yetu katika ili kuleta chachu ya maendeleo.