Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Shirika la Reli Tanzania

WANANCHI MKOANI MOROGORO WASISITIZWA KUTUMIA FEDHA ZA FIDIA KWA KIUSAHIHI


news title here
04
September
2020


Wananchi wa Kata za Pangawe, Yespa, Mtego wa Simba, Kihonda Kaskazini, Lukobe na Kingolwira mkoani Morogoro walipwa fidia zao ili kupisha Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa - SGR mkoani humo, hivi karibuni Septemba,2020.

Msisitizo huo umetolewa na Afisa Ardhi kutoka Shirika la Reli Tanzania - TRC Bwana Valentine Baraza kutumia fedha za fidia kwa matumizi sahihi ikiwemo kujenga nyumba bora na kununua mashamba kwa ajili ya kilimo.

Zoezi hilo limefanyika katika ofisi za kata ya Kingolwira Mkoani Morogoro ambapo wananchi wa kata hizo walikusanyika hapo na zoezi la kuwalipa fidia lilianza ambapo Maafisa wa Shirika la Reli, Watendaji na Wenyeviti wa kata hizo walishiriki kikamilifu ili wananchi wote wanaostaili kulipwa fidia zao kwa wakati.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Tanki la Maji kata ya Kingolwira Bwana Hassan Abdullah amelishukuru Shirika kwa kuwalipa Fidia wananchi wa kata hizo ”sikutegemea kama TRC mngekuja mapema hivi tulijua itachukua muda ukizingatia kwa sasa serikali yetu ya awamu ya tano imeanza rasmi Kampeni za uchaguzi na leo Serikali imefanya kampeni Morogoro na Mama Samia, kweli serikali ya awamu hii imejipanga vizuri “ alisema Bwana Hassan.

Naye kwa Mhandisi Msimamizi wa Kipande hicho Bwana Wambura amesema kuwa “kwa wiki mbili zilizopita tumekuwa tukipata malalamiko mengi ya wananchi nadhani sasa tumekamilisha suala hivyo wananchi wote mliolipwa leo fidia zenu tunawaomba mkaondoe nyumba zenu kama tulivyokubaliana ili mkandarasi akabidhiwe kipande hicho” alisema Mhandisi Wambura

Vivo hivyo Wananchi wa kata hizo wameishukuru TRC na kuahidi kutumia fedha za fidia kwa matumñizi husika kama yaliyopangwa na sio kutumia kwa matumizi mengine kwani kwa kutokufanya hivyo unaweza ukakosa makazi na kubaki kwenye umasikini.